Mkalimani ‘feki’ katika hafla ya
kumbukumbu ya Mandela aomba
radhi, Adai alilazwa kwenye
hospitali ya vichaa kwa mwaka
mzima.
Mkalimani wa alama za viziwi katika hafla ya
kumbukumbu ya Mandela iliyofanyika Jumanne
wiki hii (Dec 10) afahamika. Anaitwa Thamsanqa
Jantjie, 34. Mkalimani huyo ameomba radhi kwa
kile kilichotokea baada ya kushtukiwa kuwa
ishara alizokuwa anazitoa wakati wa hotuba za
viongozi hazikuwa na maana yoyote bali alikuwa
anarusha mikono tu.
Kwa mujibu wa Mail Online, Jantjie (34)
amesema anaiweza vizuri kazi hiyo lakini siku ya
kumbukumbu ya Mandela alianza kusikia
makelele kichwani kwake yaliyosababisha aanze
kutoa ishara zisizo na maana wakati wa hafla
hiyo.
Mr Jantjie ameomba radhi kwa tukio hilo na
kuongeza kuwa hakujua kilichosababisha hali
hiyo imtokee,lakini amekiri kuwahi kulazwa
hospitali ya vichaa kwa zaidi ya mwaka mmoja.
“’There was nothing I could do. I was alone in a
very dangerous situation. I tried to control
myself and not show the world what was going
on. I am very sorry. It’s the situation I found
myself in.” Mr Jantjie aliliambia gazeti la Star
newspaper la Johannesburg.
Aliongeza kuwa “What happened that day, I see
angels come to the stadium … I start realizing
that the problem is here. And the problem, I
don’t know the attack of this problem, how will it
comes. Sometimes I react violent on that place.
Sometimes I will see things that chase me,”.
Jantjie akizunguzma nyumbani kwake
Bramfischerville, South Africa, jana (Dec. 11,
2013)
Ameongeza kuwa licha ya kujigundua alikuwa
kwenye hali ngumu, lakini alijitahidi asipanic
kutokana na ulinzi mkubwa uliokuwa
umemzunguka, kwasababu hakutaka kuiaibisha
nchi yake.
Mkalimani huyo amedai kwamba alifanya kazi na
kampuni iitwayo SA Interpreters iliyopewa kazi
na ANC kwa ajili ya hafla ya kumbukumbu ya
Mandela, iliyohudhuriwa na viongozi wa mataifa
mbalimbali akiwezmo Rais wa Marekani Barrack
Obama katika uwanja wa FNB, Johannesburg
Jumanne wiki hii.
Shirika la habari la AP lilipojaribu kumuonesha
video clip ya tukio hilo wakati anatafsiri katika
memorial service ya Mandela, Jantjie alisema
hakumbuki chochote alichooneshwa katika video
hiyo licha ya kuwa ni yeye aliyekuwa
anakalimani,”I don’t remember any of this at all”,
alisema.
Mr Jantjie amesema alilipwa dola 85 (135,000
Tsh) kwaajili ya kukalimani siku hiyo. Mr Jantjie
amedai kuwa ukalimani ndiyo kazi yake ya kila
siku inayomuingizia kipato.
SOURCE: MAIL ONLINE
Friday, December 13, 2013
Mkalimani ‘feki’ katika hafla ya kumbukumbu ya Mandela aomba radhi, Adai alilazwa kwenye hospitali ya vichaa kwa mwaka mzima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment