Friday, December 13, 2013

PICHA NA STORI YA MAJAMBAZI YALIYOUWANA YENYEWE KWA YENYEWE KWA SABABU YA SHILINGI MILIONI 9 JIJINI DAR


Mwili wa Jambazi alieuwawa akiwa na kofia ya
kuendeshea pikipiki.
Pikipiki iliyotumiwa na majambazi
Mwanajeshi aliejeruhiwa.
Kuhusu hili tukio, Kamanda wa Polisi Kinondoni
anasema ‘December 11 2013 saa nane mchana
maeneo ya Maringo roundaboutJaphet Mriga
ambae ni Mwanajeshi wa JWTZ Lugalo akiwa na
mwenzake ambae ni mfanyabiashara Abdul
Zacharia, walikua wanatoka bank ya NMB
Mlimani City ambapo Mwanajeshi huyu alichukua
shilingi milioni tisa kwa dhumuni la kumpatia
Zacharia ili amnunulie gari Zanzibar’
‘Sasa walipofika maeneo ya Maringo walivamiwa
na Majambazi watatu wakiwa na pikipiki na
walifanikiwa kumpora Mriga fedha na katika
purukushani walimjeruhi Mwanajeshi huyu kwa
risasi kwenye paja na kiganjani, wakati yote hayo
yakiendelea Majambazi hawa walipigana risasi
wao kwa wao ambapo jambazi mmoja alipigwa
risasi kwenye mbavu upande wa kulia na kufariki
papohapo na kupatikana akiwa na bastola moja
yenye risasi 6′ – Kamanda
Kwa kumalizia, Kamanda amethibitisha
kukamatwa kwa pikipiki moja iliyokua ikitumiwa
na Majambazi ambapo msako mkali unaendelea
kuwatafuta wale Majambazi wengine waliotoroka
wakiwa na silaha nyingine ambayo ndio
imemuua Jambazi mwenzao na kumjeruhi
Mwanajeshi Mriga ambae alipata matibabu
hospitali ya Lugalo na sasa anaendelea vizuri.
Mwili wa Jambazi alieuwawa akiwa na kofia ya
kuendeshea pikipiki.
Wananchi wakishangaa kwenye eneo la tukio.
Gari ya Polisi ikichukua mwili wa Jambazi
pamoja na kumbeba Mwanajeshi aliejeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

.