Friday, December 13, 2013

MPASUKO FAMILIA YA MANDELA


Stori: Mwandishi Wetu na mitandao
HOFU kuu iliyopo sasa nchini Afrika Kusini
kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza
mweusi, Nelson Mandela ‘ Mzee Madiba ’ ni
kupasuka kwa familia yake baada ya mazishi
yatakayofanyika kesho kijijini Qunu , Eastern
Cape Mkoa wa Mthatha.
Baadhi ya wananchi nchini humo
wameonesha wasiwasi wao kuhusu hatima
ya mjane wa marehemu Mandela, Graca
Machel kwamba, huenda akatengwa kutokana
na umbali wa ujamii .
Graca ni mzaliwa wa Msumbiji . Aliwahi kuwa
mke wa Rais wa Kwanza wa Msumbiji ,
hayati Samora Moses Machel. Pia amewahi
kuwa Waziri wa Elimu wa Msumbiji.
Mandela akiwa na Graca .
HAKI YA KUMILIKI MALI
Mtandao mmoja nchini humo ulidai kwamba,
haki ya kumiliki mali za marehemu ipo kwa
msemaji mkubwa wa familia ya Mandela ,
Mandla Makgatho Mandela ( 39 ) ambaye ni
mjukuu wa kwanza wa marehemu.
Mandla ndiye aliyekabidhiwa mwili wa
marehemu na wanajeshi waliobeba jeneza
siku ulipopelekwa kwenye Jengo la
Muungano, Pretoria nchini humo .
Mbali na dereva , mtu mwingine aliyekuwa
ndani ya gari lililobeba jeneza ni Mandla .
Mandela akiwa na Winne .
SIFA YA MANDLA
Mandla anatajwa kuwa msemaji mwenye
mamlaka ya kufanya lolote kutokana na
wadhifa wake huo ambao hautenguliki kimila .
Hata marehemu alilijua hilo.
MASWALI YA WATU
Maswali mengi ya wakazi wa nchi hiyo ni
kama Mandla ataweza kumchukulia Graca
kuwa ni mjane sahihi anayestahili kupata
haki sawa .
Mandla ( katikati) akiwa na familia.
KUMBUKUMBU
Kabla ya kifo cha Mandela , Mandla aliwahi
kuingia matatani na baadhi ya watoto wa
marehemu kufuatia kitendo chake cha
kuhamisha miili ya marehemu wa ukoo huo
kutoka Qunu kwenda kuizika upya anakoishi
hali iliyotafsiriwa kuwa , alitaka Mandela akifa
akazikwe huko Nvezo .
Ndugu mbalimbali walikuja juu na kumtaka
arudishe miili hiyo Qunu la sivyo sheria
ingetumika .
“Hatudhani kama Mandla ataweza kumbeba
Graca kama mjane sahihi wa Mandela , wala
hatudhani kama familia hiyo itasimama kwa
amani baada ya kifo cha Madiba , ” ilisema
sehemu ya mtandao huo ikimkariri mmoja
wa raia wa nchi hiyo .
UWEPO WA WINNIE WATIA SHAKA
Habari zaidi zilidai kuwa , uwepo wa Winnie
Mandela ambaye aliwahi kuwa mke wa
marehemu kabla ya kutengana baada ya
kutoka jela mwaka 1990, ni chachu ya
kuweza kuwepo kwa mpasuko huo kwa
sababu ana watoto ambao hawaungi kizazi
cha Mandla .
Mandla alizaliwa kwa mke wa kwanza wa
Mandela, Evelyn Mase Mandela hivyo ni rahisi
uzao wa Winnie kuwa na msimamo tofauti na
msemaji huyo.
NGUVU YA WINNIE NA GRACA
Nchini Afrika Kusini, Graca ametokea kuwa na
nguvu zaidi ya Winnie akichukuliwa kuwa
ndiye aliyemtunza mzee Madiba katika
kipidni chake cha uzee, kutoka gerezani hadi
kifo.
Winnie, yeye zaidi ya kuwa katika harakati za
kupigania uhuru wakati Mandela akiwa
gerezani, alichafuka na skendo yake ya usaliti
hivyo kukosa mvuto kwa jamii ya nchi hiyo .
MANDELA ANAZIKWA KESHO
Merehemu Mandela atazikwa kesho kijijini
kwake, Qunu ambako maelfu ya watu
wanatarajiwa kuhudhuria.

No comments:

Post a Comment

.