Mwalimu Gloria Tarimo ‘ Ticha Gloria’ ( 29 )
aliyekuwa akifundisha katika Shule ya Mbezi
High School ya jijini Dar , amefariki dunia
katika mazingira ya kutatanisha huku baadhi
ya ndugu , jamaa na marafiki wakidai kifo
chake ni cha kimiujiza .
Ticha Gloria ambaye alikuwa akikaimu nafasi
ya mwalimu mkuu wa shule hiyo , alifariki
dunia Desemba 6, mwaka huu katika
Hospitali ya Muhimbili jijini Dar huku wengi
wakihisi kuna mkono wa mtu nyuma ya kifo
hicho.
Marehemu Glory A Tarimo enzi za uhai
wake.
USHIRIKINA WAHUSISHWA
Akizungumza na gazeti hili , mmoja wa ndugu
wa marehemu aliyeomba hifadhi ya jina lake
kwa kuwa si msemaji wa familia alisema , kifo
cha Ticha Gloria kinahusishwa na ushirikina
kwa kuwa kabla ya mauti kumfika
alikumbana na mambo mengi ya ajabu .
“Ni kifo cha ajabu kwa kweli na
kimemshangaza kila mmoja wetu.
Nakumbuka ilikuwa Juni, mwaka huu ambapo
alienda kazini na alipofika kwenye mlango wa
ofisi yake alikuta nazi imevunjwa .
“Licha ya kushangazwa na uwepo wa nazi
hiyo , aliiruka kisha akaingia ofisini kwake.
Kuanzia hapo alianza kuumwa mguu , kuna
wakati akawa anahisi unawaka moto.
Tulimpeleka Hospitali ya Muhimbili ,
akapatiwa matibabu na akapata nafuu , ”
alisema ndugu huyo.
AKUTA NJIWA KWENYE KITI OFISINI
Ndugu huyo alizidi kueleza kwa masikitiko
kuwa , baada ya tukio hilo la kukuta nazi
imevunjwa kwenye mlango wa ofisi yake,
mambo hayakuishia hapo kwani hivi karibuni
alipoingia ofisini kwake alikuta Njiwa kwenye
kiti chake .
“Alipiga kelele sana , walimu na wanafunzi
wake wakaja kushuhudia huku kila mmoja
akishangaa na kuogopa kumtoa njiwa yule
kwenye kiti.
“Mwalimu mmoja aliyefahamikwa kwa jina la
Fadhili ndiye aliyemuondoa njiwa yule . Bila
kujua kuwa roho yake inasakwa , Gloria
akakaa kwenye kile kiti na kuendelea na
shughuli zake , ” alisema ndugu huyo na
kuongeza :
“Haikuchukua muda mrefu akahisi kama
anachomwa na kitu chenye ncha kali kwenye
makalio yake huku kichwa kikimuuma sana.
Walimu wenzake walimchukua na kumrudisha
hospitalini. ”
AANZA KUZIONA SIKU ZAKE MFULULIZO
Ilielezwa kuwa , baada ya mwalimu Gloria
kufikishwa hospitalini , hali ilizidi kuwa mbaya
na akaanza kutokwa na damu ya hedhi
mabongemabonge huku damu nyingine
ikitokea puani .
Ndugu wa Marehemu.
“Hali ilikuwa hivyo , akawa anateseka sana
huku wakati mwingine akilalamikia baadhi ya
walimu wenzake kuwa ndiyo wanaotaka
kumtoa roho.
“Kuna siku alimuita daktari aliyekuwa
akimhudumia na kumwambia anamshukuru
kwa kujitahidi kuokoa uhai wake lakini
anaamini hatapona kwani anajua kuna
walimu wamedhamiria kumuua ili wakalie kiti
cha ualimu mkuu , baada ya hapo alikata
roho,” alisema ndugu huyo ambaye ndiye
aliyekuwa akiwasiliana na marehemu mara
kwa mara.
WALIMU WANASEMAJE ?
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati
tofauti , baadhi ya walimu wa shule hiyo
walisema wamesikitishwa sana na kifo cha
Ticha Gloria, wakasema licha ya kwamba kila
kifo kinapangwa na Mungu lakini hiki cha
mwenzao kimeacha utata .
“Kwa kweli kifo cha Gloria kimenifanya
niamini kuwa Mungu yupo lakini pia
ushirikina upo . Amekufa kifo cha kimiujiza
sana, mambo yaliyomtokea kabla ya kufariki
dunia yanaashiria kabisa kuna mkono wa
mtu, ” alisema mwalimu mmoja wa kike
aliyeomba hifadhi ya jina lake.
MSIKIE MWENYE SHULE
Mkurugenzi wa shule hiyo aliyefahamika kwa
jina la Said Mgude alielezea masikitiko yake
juu ya kifo cha mwalimu Gloria kwa kuwa
alikuwa mchapakazi sana ila akataka watu
wasihusishe kifo hicho na mambo ya
kishirikina .
“Kila mmoja lazima aumie kwa kifo cha
Gloria, lakini nawasihi watu wamuamini
Mungu na waachane na dhana za kishirikina .
Shule yangu ni taasisi kubwa sana, minazi
ipo mingi hivyo kama alikuta nazi imevujwa
mlangoni inawezekana ilianguka tu na
kupasuka .
“Kuhusu Njiwa hapa Dar es Salaam siyo
jambo la ajabu kwa sababu wapo wengi
sana, mimi siwezi kukubaliana na mambo
hayo ya kishirikina na hakuna kitu kama
hicho,” alisema .
Mwili wa mwalimu Gloria uliagwa Desemba
10, mwaka huu katika Kanisa Katoliki Mbezi
Mwisho jijini Dar na baadaye ulisafirishwa
kwenda Moshi Rombo mkoani Kilimanjaro na
kuzikwa siku iliyofuata ya Desemba 11 .
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali
pema peponi-Amin .
Friday, December 13, 2013
MWALIMU AFA KIMIUJIZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kazi ni mzigo wa mwiba
ReplyDelete