"Kazi kijeba" picha hii ni ya schache
zilizopita baada ya kuchezea kichapo
kutoka kwa huyo mpezi wake wa zamani
walioachana.
MSANII huyu amekuwa mgumu wa kuelewa kila
akielezwa na uongozi wa kampuni ya Al-riyamy
Production na wasanii wenzake kwa ujumla
kuwa apunguze unywaji wa pombe kupita kiasi
hadi kubebwa na wananchi wenye huruma
kuletwa kambini yeye huitikia na
kukiri kwamba hatorudia lakini hazipiti siku
mbili lazima usikie kalewa kaenda kumtukana
mpenzi wake walioachana..!
Hivi majuzi aliripotiwa kambini na muendesha
baiskeli (bodaboda) kwamba alimkodi
akamwambia ampeleke Usagara maeneo
akanywe bia mara bodaboda anashangaa
anaelekezwa mitaa isio na dalili yeyote ya
kuuzwa bia..!
Ghafla wakafika kwenye nyumba flani
wakamkuta dada na mpenzi wake wametulia nje
kwao wanapunga upepo, Ndipo Msanii
aliposhuka kwenye baiskeli nakuanza
kumporomoshea matusi ya nguoni yule dada na
mpenzi wake huku akijitapa kwamba yeye ana
ukimwi na kashamuambukiza huyo mwanamke
kwahiyo huyo mpenzi wake mpya ajiandae kufa
kwa gonjwa hatari la ukimwi...!,
Dada huyo ambaye alikuwa mpenzi wake kweli
enzi hizo lakini kwasasa walishatengana
aliamua kupiga simu kwa mmoja kati ya
wasanii waVITUKO SHOW na kutoa malalamiko
yake usiku huohuo Akakiri kutokurudia
sualahilo Wasanii wenzake baada ya kufikishiwa
taarifa hiyo na muendesha baikeli pamoja na
simu iliyopigwa na dada huyo wamkalisha chini
tena Kazi chini kama kawaida na kumuonya,
Akakiri kutokurudia suala hilo. Amakweli siko la
kufa halisikii dawa..!
Cha ajabu jana kalewa tena na kuenda
kumtukana dada huyo tena, Dada akaenda
kuripoti polisi leo wamemtia mbaroni Kazi A.k.a
Kijeba yupo kituo cha polisi makorora mkoani
Tanga anasubiri kupanda mahakamani
Jumatatu tarehe 9- December 2013 kusomewa
mashtaka. Fatilia raarifa zaidi hapa katika
website yako ya kijajnja
Saturday, December 7, 2013
MSANII WA KUNDI LA VITUKO SHOW BAADA KUCHEZEA KICHAPO CHA PAKA MWIZI SIKU ZA KARIBUNI SASA ASWEKWA RUMANDE MKOANI TANGA..! SOMA KISA UCHEKE MWENYEWE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hahaha alikua anaham ya mahabusu
ReplyDelete