Wednesday, December 4, 2013

MWINGIRA ABURUZWA KORTINI..TUHUMA ZA KUZAA NA MKE WA MTU


Stori: Wandishi Wetu
LILE sakata la Nabii na Mtume Josephat
Mwingira kudaiwa kuzaa na mke wa mtu Dk.
Phills Nyambi limeendelea kupamba moto,
mlalamikaji Dk. Morris William, raia wa Liberia
amefungua kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es Salaam, akidai fidia ya shilingi
bilioni 7.5.
Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Dk. William,
anayewakilishwa na Wakili Desidery Ndibalema
amemshitaki Mwingira kama mlalamikiwa namba
moja na mke wa mlalamikaji, Dk. Philis Nyimbi ni
mshtakiwa wa pili.
Tayari shauri hilo lililopelekwa mahakamni
Novemba 21, mwaka huu na kupewa usajili
namba 306 la 2013 limepangwa kutajwa
Desemba 12, mwaka huu na hakimu
atakayelisikiliza ni Hakimu Mkazi Hellen Riwa.
Chanzo chetu ndani ya Mahakama ya Kisutu,
kimesema kuwa katika nyaraka za mashtaka
(nakala tunazo) zilizowasilishwa mahakamani
hapo, Dk. William amedai kuwa katika tarehe
ambayo haijulikani Mwingira aliingia katika
uhusiano wa kimapenzi na mkewe.
Nyaraka hizo zinaeleza kuwa baada ya
mlalamika kugundua kuhusu hilo, alimuuliza
mkewe ambaye alijitetea kwamba alibakwa.
Zinaeleza kuwa uhusiano huo haukuishia katika
kupewa mimba tu bali pia mke wake kupata
changamoto nyingine za kiafya ambazo hata
hivyo hakuzitaja.
HOJA YA WAKILI WA MLALAMIKAJI
Katika nyaraka hizo, Wakili Ndibalema alisema
kuwa mteja wake baada ya kubaini kwamba
mkewe amezaa na Mwingira, vilevile amepata
changamoto za kiafya, aliamua kutoa ripoti Kituo
cha Polisi Kati, Kibaha, Pwani.
“Polisi walimjibu mteja wangu kuwa hiyo ni kesi
ya madai, siyo jinai, wakamshauri afungue
madai mahakamani,” anaeleza Ndibalema
kwenye hati hiyo ya mashtaka.
Anaendelea kusema, mtoto ambaye Mwingira
analalamikiwa kuzaa na Dk. Philis ana umri wa
miaka mitano hivi sasa.
Wakili Ndibalema anaeleza: “Uhusiano huo wa
kimapenzi, umesababisha usaliti katika ndoa ya
halali ya mteja wangu, imemsababishia kukata
tamaa ya maisha na kuathirika kisaikolojia.
“Uwezo wa utendaji kazi wa mteja wangu
umeshuka kwa kiwango kikubwa, anaongoza
taasisi isiyo ya kiserikali ya kimataifa ambayo
sasa imekosa udhamini kutoka kwa mtu mmoja
mmoja au vikundi vya taasisi mbalimbali
duniani.
“Kwa hatua hiyo, mteja wangu amevunjiwa
heshima na kushushwa hadhi yake siyo Tanzania
tu bali duniani kote.”
ANACHOHITAJI DK. WILLIAM KWA MWINGIRA
Katika maelezo yake, Dk. William anaomba
kupitia kwa wakili wake kwamba mahakama
iamuru yeye, Dk. Philis na Mwingira, wakapimwe
Ukimwi na mtoto afanyiwe uchunguzi wa DNA.
Dk. William pia amedai kuwa ana vifaa vya
hospitali vyenye thamani ya dola za Kimarekani
6,500,000 (zaidi ya shilingi bilioni 10), ambavyo
Mwingira amevichukua baada ya kula njama na
Dk. Philis.
ANAOMBA ALIPWE SHILINGI BILIONI 7.5
Katika hoja hiyo, Dk. William anaomba kwanza
arudishiwe vifaa vyake ambavyo amedai
Mwingira na Dk. Philis kuvitaifisha na baada ya
kurejeshewa, alipwe fidia ya shilingi bilioni 7.5.
Dk. William ametoa hoja ya kwa nini alipwe
kiasi hicho kwamba; yeye ni mtaalamu wa
kimataifa wa afya ambaye amewahi kutambuliwa
na Ikulu ya Marekani (White House) chini ya
marais Bill Clinton na George Bush.
Taasisi yake iitwayo Global 2000(2010)
International ambayo imejikita Texas, Marekani
ilitambuliwa na Umoja wa Mataifa na alibuni
vifaa mbalimbali vya matumizi katika sekta ya
afya na magari nchini Marekani ambavyo
thamani yake ni dola za Kimarekani 100,000,000
(zaidi ya shilingi bilioni 160).
Alikuwa na mpango kwa kushirikiana na mkewe
kujenga kituo cha utafiti cha afya na hoteli ya
nyota tano mkoani Kilimanjaro na alinunua
hekari 37 kwa ajili hiyo, hata hivyo, mkewe
alimpa Mwingira zawadi.
Alichaguliwa kuwa mmoja wa watu
wanaotambuliwa katika huduma za afya kwa
karne ya 21 kutokana na utendaji wake katika
tasnia hiyo nchini Marekani.
Alikuwa akiishi vizuri na mkewe na alishaanza
kumtafutia viza ili aweze kwenda kufanya naye
kazi na kuishi Marekani.
DK. WILLIAM AZUNGUMZA
Dk. William alipotafutwa na waandishi wetu
alikiri kufungua kesi hiyo, akasema:
“Nina mpango wa kumfulia Mwingira kesi
nyingine ya madai katika mahakama ya
kimataifa kama nitaona hapa Tanzania sitendewi
haki.”
MWINGIRA JE?
Kwa upande wa Mwingira bado ni vigumu
kumpata, kwani jitihada za waandishi wetu
kumtafuta kuzungumza naye hazikuzaa
matunda, kwani zilikwamishwa na wasaidizi
wake ambao hawataki kabisa bosi wao ahojiwe

No comments:

Post a Comment

.