Monday, December 16, 2013

NAY: SIWEMA AKINIBAMBA NA MADEMU ANAZIMIA


STAA wa muziki wa kizazi kipya Bongo,
Emmanuel Elibariki ‘ Nay wa Mitego ’ , hivi
karibuni alifunguka kuwa hakuna jambo
analoepukana nalo kama kukutwa na
mchumba wake, Siwema akiwa na mademu
wengine maana huwa anazimia.
Akipiga stori na paparazi wetu Desemba 13,
mwaka huu , Nay alisema kwamba pamoja na
usanii wake wote na kuwa karibu na
mashabiki wa muziki wake , amekuwa
akijiepusha sana kwenye suala zima la kuwa
karibu na mademu kwani hapendi
kumsababishia Siwema matatizo ya kuzimia .
“Mchumba wangu ananipenda sana na ndiyo
maana sasa ninaishi kwa tahadhari kubwa
kwani sipendi kumuona Siwema wangu
akizimia kwa sababu ya wivu , najitahidi
kumlinda kwa kujiepusha kuwa karibu na
mademu , ” alisema Nay.

No comments:

Post a Comment

.