Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE historia imeandikwa , Mzee Nelson
Mandela, rais wa kwanza mweusi wa Afrika
Kusini amezikwa jana katika shughuli kubwa
iliyoshuhudiwa na mamilioni ya watu duniani
kote kupitia runinga huku picha ya mwili
wake ukiwa ndani ya jeneza ikiwa ndiyo dili
kubwa .
Mazishi ya Mzee Madiba aliyefariki dunia
Desemba 5, 2013 yalifanyika katika kijiji
alichokulia , Qunu , Mkoa wa Mthatha katika
Jimbo la Eastern Cape nchini humo .
Wiki iliyopita , serikali ya Afrika Kusini ilitoa
amri kwamba haruhusiwi mtu yeyote kupiga
picha ya mwili wa marehemu akiwa anaagwa
jijini Pretoria.
Picha ya Mandela akiwa kwenye jeneza .
Familia nayo ikapigilia msumari wa mwisho
ikisisitiza kuwa , binadamu yeyote mwenye
akili timamu haruhusiwi kupiga picha ya
mwili huo ukiwa ndani ya jeneza .
Amri hiyo ilivivunja nguvu vyombo mbalimbali
vya habari duniani ambavyo vilikuwa nchini
humo vikifuatilia mazishi na maziko ya
Mandela.
Serikali iliweka wazi kwamba , mtu yeyote
atakayepiga picha, akinaswa zitafutwa
kwanza halafu kama ni Msauzi atashitakiwa
na kama ni raia wa nje atarudishwa nchini
mwake na kupigwa marufuku kuingia nchini
humo maishani mwake .
Baadhi ya watu nchini humo wamekuwa
wakihaha kupata picha hiyo ili waitengenezee
fremu na kuiingiza sokoni kwa wanunuzi .
Juzi , baadhi ya mitandao iliweka sehemu ya
sura ya Mandela na kudai ni picha yake
akiwa kwenye jeneza siku chache baada ya
kifo.
Hata hivyo , haraka sana, baadhi ya vyombo
vya usalama nchini humo vilikanusha na
kusema picha hiyo ni enzi za uhai wake
akiwa amelala.
Ukawekwa ushahidi wa picha hiyo ikiwa yote
ambapo Mzee Madiba alikuwa akiuchapa
usingizi wakati fulani enzi za uhai wake .
Kuhusu maziko yake, zaidi ya wageni 4, 500
kutoka pande zote za dunia walihudhuria
ndani ya hema kubwa lililojengwa katika eneo
la familia ya Mandela huku mamia ya
wanakijiji na baadhi ya wanafamilia
wakikosa nafasi ya kuuaga mwili wa
mpendwa wao huyo.
Idadi kubwa ya viongozi waliohudhuria ,
wakiwemo Rais Barak Obama wa Marekani
na mtoto mkubwa wa Malkia wa Uingereza,
Prince Charles, kumelifanya eneo la kijiji hicho
kuwa dogo na linalohitaji uangalizi wa hali ya
juu wa usalama . Katika kuhakikisha kila kitu
kinakwenda sawa kiusalama, ndege mbili za
jeshi la nchi hiyo zilikuwa angani pamoja na
helikopta kadhaa.
Zaidi ya wanajeshi 20, 000 walilinda usalama
katika kijiji hicho wakifanya kazi sambamba
na jeshi la polisi .
Licha ya wenyeji na majirani hao wa
marehemu Mandela kunyimwa fursa ya
kuuaga mwili huo , pia walizuiwa kuukaribia
kutokana na uhaba wa nafasi, kitendo
ambacho kililalamikiwa sana.
Waliokosa nafasi ya kuhudhuria mazishi hayo
siyo tu majirani, bali hata mtoto wa kaka
mkubwa wa Mandela , Maurice aitwaye
Mzwandile Mandela mwenye umri wa miaka
13.
Mwingine ni mpwa wa Mandela , Gloria
Mkwedini, mtoto wa dada yake ambaye pia
hakuhudhuria mazishi hayo pamoja na
familia yake ya watu 16.
Watu hao wanaishi maili chache kutoka kwa
Madiba wakiwa wanaishi katika moja ya
nyumba nyingi za mduara zilizoko katika
eneo hilo.
Na kwa vile hakuna umeme, hawakuweza
kufuatilia tukio hilo katika televisheni.
‘ Hii imetufanya tujione kama ni watu wageni
tuliotengwa,” alisema Gloria akimlaumu
mtoto mkubwa wa kike wa Mandela ,
Makaziwe, 59 , aliyedai kuwa ndiye aliyekuwa
anaamua nani aalikwe na nani aachwe .
Alisema mume wake alimfuata Makaziwe na
kutaka kupewa mwaliko , lakini binti huyo
alikataa . Alilalamika kuwa kunyimwa kwao
mwaliko kunatokana na umasikini wao .
Mandela alizikwa kimila , kwa ndugu wa
karibu wa familia yake pamoja na viongozi
wa kimila wapatao 70 waliokabidhiwa mwili
huo na kuuingiza ndani ya nyumba yake ya
milele huku pia wakikataa tukio hilo kurushwa
na chombo chochote cha habari.
Miongoni mwa mila na desturi za kabila la
Mandela linalofahamika kwa jina la Aba
Thembu ni pamoja na kuchinjwa kwa
ng’ ombe dume aliyenona na damu yake
kumwagiwa ndani ya kaburi la marehemu.
Taifa la Afrika Kusini limekuwa lenye
pilikapilika nyingi tangu kufariki dunia kwa
mpigania haki huyo Desemba 5, mwaka huu ,
nyumbani kwake jijini Johannesburg baada
ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa
mapafu.
Mwili wake uliondolewa saa tisa usiku na
kupelekwa katika hospitali ya kijeshi jijini
Pretoria ambako kwa siku tatu kuanzia
Jumatano , uliwekwa katika majengo ya Ikulu
ambako zaidi ya watu laki moja waliripotiwa
kuuaga.
Hata hivyo , serikali ilitoa amri ya kusitishwa
kwa shughuli hiyo huku maelfu ya wananchi
wakiwa katika msururu mrefu wakisubiri
kupata nafasi ya kumuaga mtu
anayedhaniwa kuwa ndiye maarufu na
mwenye heshima zaidi kuliko wote katika
karne ya 21 .
Monday, December 16, 2013
PICHA YA MANDELA AKIWA KWENYE JENEZA YAWA DILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment