Tuesday, December 10, 2013

RAISI JAKAYA KIKWETE AMETOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 1,475.AKINA NANI HAO??....BOFYA HAPA


Katika kuadhimisha miaka 52 ya uhuru wa
Tanganyika rais Jakaya Kikwete ametoa
msamaha kwa wafungwa 1,475.
Taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya
ndani ya nchi Mh. Emmanuel Nchimbi imesema
wafungwa watakaonufaika na msamaha huo wa
rais ni wale wagonjwa wa Ukimwi, kifua kikuu
na saratani ambao wako kwenye hali mbaya.
Wengine ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 70
walioingia kifungoni na mimba na wale wenye
watoto wachanga na wale wenye ulemavu wa
mwili na akili.
Aidha msamaha huo wa raia hautawahusu
waliohukumiwa kunyongwa au wanaotumikia
kifungo cha maisha, wanaotumikia kifungo
kutoka na makaosa ya biashara ra ya dawa za
kulevya , rushwa, wizi na unyang’anyi wa
kutumia silaha , waliobaka, kunajisi au kulawiti,
wezi wa magari na wale waliowapa mimba
wanafunzi.
Wengine ni wale waliofungwa kwa matumizi
mabaya ya madaraka na wale waliowahi
kutoroka wakati wa kifungo.
-Mpekuzi

No comments:

Post a Comment

.