Friday, December 13, 2013

SWALA LA SHAA KUWA MJAMZITO..!! HATIMAYE SHAA AUNGUKA NA KUSEMA HAYA KUHUSU UJAUZITO..!!


Sarah Kaisi aka Shaa bado ana siku nyingi za
kula ujana wake kama Nay wa Mitego sababu
hategemei kuwa mama siku za hivi karibuni
kama wengi walivyodhani kufuatia picha yake
aliyoiweka Instagram hivi karibuni inayoonesha
nguo za mtoto.
“Ni kweli niliweka picha ya nguo za mtoto zikiwa
dukani wakati nikichagua nguo za kununua kwa
ajili ya mtoto wa rafiki yangu,” Shaa aliliambia
gazeti la Mwanaspoti.
“Lakini ile haina maana kwamba ninatarajia
kupata mtoto, unapoandika kitu haina maana
kwamba umesimama katika hilo inaweza kuwa
kwa upande mwingine pia. Ni kama ilivyokuwa
katika suala la picha hiyo.”

No comments:

Post a Comment

.