Kijana mmoja ambaye hajatambulika jina lake
mwenye umri kati ya miaka 26 hadi 30 ameuawa
kwa kupigwa risasi wakati akiwa na wenzake
wakijaribu kuvunja duka maeneo ya Shunu, kata
ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.
Tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa
kuamkia leo ambapo jambazi hilo likiwa na
wenzake watatu liliuawa kwa kupigwa risasi
kichwani na Wilson Masolwa (63) mkazi wa
mtaa huo ambaye alijeruhiwa kwa mapanga.
Mtu huyo ameuawa kwa Bunduki aina ya
Shortgun ambayo hata hivyo wenzake waliipora
baada ya kumkata mapanga Masolwa na
kupoteza fahamu.
Akizungumzia tukio hilo mmiliki wa nyumba hiyo
Yasinta Patrick (32) amesema mtu huyo na
wenzake walivamia katika nyumba yake, ambayo
ameipangisha kwa wafanyabiashara wawili wa
kutoa na kutuma fedha kwa njia ya mtandao.
Yasinta ambaye pia amejeruhiwa kiasi amesema
lengo la majambazi hao lilikuwa ni kuiba pesa
katika maduka hayo baada ya kumfuata katika
chumba kingine alichokuwa amelala na kumpiga
huku wakimtaka atoe pesa za biashara hiyo.
Kwa upande wake Masolwa amesema baada
kusikia kelele alifika katika eneo la tukio na
ndipo majambazi hao walianza kumkata
mapanga kabla ya yeye kumpiga risasi ya kichwa
mmoja wao na kufariki dunia papo hapo.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
ACP Kihenya Kihenya amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba Masolwa amefikishwa
katika Hospitali ya wilaya ya Kahama kupatiwa
matibabu na kuruhusiwa na kwamba hali yake
inaendelea vizuri.
Kamanda Kihenya mwili wa marehemu huyo
umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya
Kahamaa na kwamba jeshi la polisi linaendelea
na msako wa kuwabaini na kuwakamata
wahusika watatu waliotoroka ikiwa ni pamoja na
bunduki waliyoipora.
Thursday, December 5, 2013
TAHADHARI PICHA ZINATISHA: JAMBAZI LAUAWA KWA RISASI WILAYANI KAHAMA...!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment