Wednesday, December 4, 2013

TFF YAMNYIMA MKATABA MPYA MZUNGU WA KUWAPIKA VIJANA


Kocha wa timu za vijana , Jacob Michelsen .
SHIRIKISHO la Soka Tanzania ( TFF ) ,
limeweka wazi kuwa halitamuongezea ajira
kocha wa timu za vijana , Jacob Michelsen
raia wa Denmark .
Uamuzi huo , umetangazwa leo na Rais wa
TFF , Jamal Malinzi, ambapo amesema
shirikisho lake limeona hakuna sababu ya
kumuongezea mkataba kocha huyo, ambao
unamalizika Desemba 15, mwaka huu.
Malinzi, amesema mara baada ya mkataba
huo wa Michelsen kumalizika , TFF itamsaka
mrithi wake, ambapo sasa Mtanzania
atachukua nafasi ya Mdenish huyo, ukiwa ni
mkakati maalum wa kuwapa wazawa nafasi.
“Tumeona hakuna haja ya kumuongezea
mkataba Jacob ( Michelsen ) , mkataba wake
wa sasa unafikia tamati Desemba 15, mwaka
huu na utakapomalizika ataondoka mara
moja na tayari tumeshamjulisha mapema juu
ya uamuzi huo , ” alisema Malinzi.
“Tumekubaliana kama TFF , kwamba mara
baada ya Jacob kuondoka nafasi yake
atafutwe kocha wa Kitanzania, mwenye
uwezo ili azibe nafasi yake , hii ni katika
kuwapa nafasi wazawa wenye uwezo wa
kufanya majukumu haya, tunajua kuwa watu
makini wapo.

No comments:

Post a Comment

.