Wednesday, December 4, 2013

ZANZIBAR HEROES YAPIGWA NA KENYA - HATARINI KUAGA MASHINDANO YA CHELLENJI


Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe.COM
MICHUANO ya kombe la Mataifa ya Afrika
mashariki na kati, CECAFA Challenge imezidi
kushika kasi leo nchini Kenya ambapo wenyeji
Kenya wameungana na
Wahabeshi wa Ethiopia kutinga hatua ya robo
fainali baada ya kuifumua Zanzibar Heroes
mabao 2-0, Uwanja wa Afrah, Nakuru.
Alikuwa ni Beki wa Azam fc, inayoshiriki ligi kuu
Tanzania bara, Joackins Atudo aliyekuwa wa
kwanza kuandika bao la kwanza dakika ya 6 na
baadaye mshambuliaji wa AFC Leopards ya
Kenya, Allan Wanga akaandika kimiani bao la pili
dakika ya 60.
Kwa matokeo ya leo, Zanzibar inabaki na alama
zake tatu na sasa wapo mguu ndani-nje kwani
watasubiri hatima ya kwenda robo fainali katika
nafasi mbili za `Best Losers`.
Kwa Harambee Stars mambo yamejipa yenyewe
kwa kutinga robo fainali kwani wametimiza
alama 7 baada ya awali kuwalaza Sudan Kusini
mabao 3-1 na kutoka suluhu na Ethiopia.
Mchezo mwingine wa kundi A uliopigwa mapema
uliwakutanisha Sudan kusini dhidi ya Ethiopia na
kushuhudia dakika tisini zikikamilika kwa
wahabeshi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0,
uwanja wa Afrah mjini Nakuru, Kenya.
Mabao ya Ethiopia yalifungwa na Yousuf Yassin
aliyetokea benchi kipindi cha pili na kufunga bao
la kwanza dakika ya 54 baada ya kupokea pasi
nzuri ya Manaye Fantu kutoka upande wa kulia
na Biruk Kalbolre aliyeingia pia kipindi cha pili na
kufunga goli muhimu dakika ya 82.
Sudani Kusini sasa linakuwa Taifa la kwanza
kutoa mkono wa `Bai Bai` katika michuano ya
mwaka huu bila hata kupata pointi moja, kwani
walifungwa mechi zake mbili za mwanzo, 2-1
dhidi ya Zanzibar na 3-1 kutoka kwa wenyeji
Harambee stars.
Kesho shughuli inaendelea kwa timu za kundi B,
ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania bara,
Kilimanjaro Stars itajitupa uwanjani katika
mchezo muhimu sana dhidi ya Burundi na
Zambia watakabiliana na mabaharia wa Somalia.
crediti-Shafiidauda

No comments:

Post a Comment

.