Wednesday, February 26, 2014

MBONGO ALIYEBAKWA HADI KUFA CHINA. .. MAZITO YAIBUKA!


Stori : Shakoor Jongo na Gabriel Ng ’ osha
KATIKA Gazeti la Ijumaa Wikienda la juzi
Jumatatu, Toleo Namba 354 ukurasa wake
wa mbele kuna habari yenye kichwa
kisemacho ; MBONGO ABAKWA CHINA, AFA !
Sabrina enzi za uhai wake .
Katika habari hiyo , kulisindikizwa na vichwa
vidogo vilivyosomeka; Wabakaji ni Wanigeria
watano , maiti yake yakutwa haina figo ,
moyo!
Habari hiyo ilimhusu Mtanzania
aliyejulikana kwa jina la Sabrina au Habiba
kwamba, aliondoka Bongo kwenda
Guangzhou, China akidanganywa na
mwanamke mmoja kwamba anakwenda
kufanya kazi kwenye saluni ya kike.
Habari zilisema baada ya kufika China,
mwanamke huyo alimnyang’anya Habiba
hati ya kusafiria na kumwingiza kwenye
biashara ya ukahaba kwa kumuuza kwa
wanaume huku ujira akiuchukua yeye.
Ilidaiwa kuwa , tabia hiyo ndiyo iliyopo kwa
sasa kwamba , kuna wasichana
wanachukuliwa kupelekwa nchini humo kwa
kudanganywa kufanya kazi saluni matokeo
yake huishia kwenye ukahaba .
NDUGU WASOMA GAZETI , WAJITOKEZA
Sasa, baada ya gazeti hilo kuingia mtaani
siku hiyo , mazito yakaibuka .
Ndugu mmoja aliyejitambulisha kuwa ni
kaka wa marehemu alimpigia simu Mhariri
Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global
Publishers , Oscar Ndauka na kumweleza
kuwa wamesoma habari za kifo cha Habiba
kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda .
Akizungumza kwa sauti iliyojaa simanzi,
ndugu huyo alisema nyumbani kwao ni
Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam.
Mhariri: Ndugu poleni sana! Je , naweza
kutuma waandishi wangu wakafika hapo na
kujua mawili matatu kuhusu marehemu ?
Ndugu: Hamna tatizo, baba yupo ila mama
alikuwa Vikindu ( Dar) ndiyo anakuja yuko
njiani.
Mhariri alituma waandishi wawili kufuatilia
mkasa huo ambao umewatikisa Wabongo
waishio eneo la Guangzhou nchini China .
WAANDISHI MSIBANI, WAKUTANA NA BABA
MZAZI
Akizungumza msibani , baba mzazi wa
marehemu , mzee Yusuf Ally alisema Habiba
aliondoka nchini kwa kutoroka kwenye
Sikukuu ya Idd El Haj mwaka 2012.
Alisema hakuwa na mawasiliano mazuri na
bintiye huyo si kwa sababu ya kutoroka tu
bali kwa vitendo alivyokuwa akivifanya na
kila alipomuonya binti huyo hakusikia,
mwishowe akaamua kukata mawasiliano
naye.
“Sikuwa na mawasiliano na Habiba tangu
Machi 2010 kwani aliniudhi sana , ” alisema
mzee huyo licha ya kwamba alikuwa
akiporomosha machozi kufuatia taarifa za
kifo cha binti yake .
NINI HASA UGOMVI WA HABIBA NA BABA
YAKE ?
Akiendelea kusimulia maisha aliyokuwa
akiishi na mwanaye huyo , mzee Yusuf
alisema:
“Habiba alibadilika tabia akawa hataki
kusoma. Mbaya zaidi kilichonikera ni pale
alipokataa kwenda kufanya mtihani wa
kumaliza kidato cha nne mwaka 2010.
Kiukweli iliniuma sana .
“Nilimsomesha kuanzia kidato cha kwanza
hadi cha nne , nilikuwa najinyima kula kwa
ajili yake, siku ya mtihani akakataa
kwenda shule , niliumia sana hasa
nikikumbuka fedha zangu nilizotupa kwa
ajili yake, ” alisema .
JINSI ALIVYOONDOKA BONGO
Naye dada wa Habiba , Aziza Said ambaye
alikuwa akiishi na marehemu alisema
kwamba ilikuwa siku ya Idd El Haj mwaka
2012 ndiyo siku ambayo mdogo wake huyo
alitoroka nyumbani na kwenda kujificha
kusikojulikana.
“Siku hiyo nilimwachia fedha ili aende
saluni akamsuke mtoto, mi nikaenda
Kariakoo . Niliporudi nikakuta fedha za
kusukia ziko mezani na mtoto anacheza
nje .
“Nilimuuliza mwanangu mama mdogo yuko
wapi? Akanijibu hajui . Sikuwa na wasiwasi
kwani nilijua alikwenda kwa mashoga zake
kula sikukuu , kwangu alihisi ningembana.
Kumbe mwenzangu yuko katika mipango ya
kutoroshwa nchini, ” alisema dada huyo na
kuangua kilio .
MWANAMKE ALIYEMTOROSHA WANAMJUA
Familia hiyo ilisema mwanamke
aliyemtorosha Habiba kutoka Bongo kwenda
China wanamjua (jina tunalo) kwani
waliwahi kuishi naye nyumba moja , Manzese
jijini Dar lakini wakawa hawaongei naye
kwa sababu ya tabia zake mbaya .
Walisema mwanamke huyo alianza
kumbadili tabia Habiba miezi michache
kabla ya safari ya China, hasa kwa mavazi
ya ajabu na tabia ya kutotulia nyumbani .
Waliendelea kusema kuwa , ilifika mahali
kutokana na tabia yake mpya isiyo na
maadili , waliamini binti huyo ametumbukia
kwenye mambo ya kigodoro ( ngoma za
uswahilini ).
MARA YA MWISHO KUONEKANA WHATSAPP
Kaka wa marehemu Mohammed Yusuf Ally
alipoongea na gazeti hili msibani hapo
alisema kuwa mara ya mwisho kufanya
mawasiliano na marehemu ilikuwa
Valentine ’s Day ( Sikukuu ya Wapendanao )
– Februari 14 , mwaka huu, ambapo
alimtumia ujumbe mfupi wa maneno katika
Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp lakini
meseji hiyo haikujibiwa .
“Nimeshtuka sana leo kupata taarifa
kwamba mdogo wangu amefariki dunia tena
baada ya kusoma gazeti (Ijumaa Wikienda )
huku kifo chake kikiwa cha kikatili kiasi
hicho , ” alisema akilia kaka huyo .
NYONGEZA NYINGINE YA TAARIFA
Kwa mujibu wa ndugu, mbali na miongoni
mwao kulisoma Gazeti la Ijumaa Wikienda
na kupata taarifa , lakini kwa mzee Yusuf
habari zilimfikia baada ya jirani kununua
gazeti hilo na kumpelekea nyumbani hapo.
KAKA AISHUKURU GLOBAL
“Nalishukuru hili gazeti ( Wikienda ) kwani
bila ya wao kuandika tusingejua nini
kinaendelea huko China, ” alisema kaka wa
marehemu huku akiwa ameshika gazeti hilo

No comments:

Post a Comment

.