Sunday, February 23, 2014

AJIUZA SIKU TATU KABLA YA KUJIFUNGUA


Stori : Chande Abdallah na Deogratius
Mongela
YELEUUUWI! Mwanamke mjamzito
aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamisa
amenaswa laivu na ‘makachero ’ wa
Oparesheni Fichua Maovu ( OFM ) ya Global
Publishers , akijiuza huku akiwa na
ujauzito wa miezi nane na siku 27, zikiwa
zimesalia siku tatu afikishe miezi tisa
tayari kwa kujifungua .
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri wiki iliyopita
usiku wa manane Mbagala - Zakhem, Dar,
wakati OFM ikiwa katika oparesheni zake
kwenye danguro moja maarufu
linalojulikana kwa jina la Kwaswai lililopo
maeneo hayo .
OFM ikishirikiana na polisi wa Kituo cha
Mbagala - Kizuiani ilifumuafumua danguro
hilo na kuwanasa watu kadhaa wakifanya
vitendo haramu na hatarishi vya ngono
lakini kilichowastaajabisha na kuwaacha
midomo wazi watu waliofurika katika eneo
hilo, ni mmoja wa machangu hao kunaswa
akiwa na ujauzito .
Akizungumza na OFM baada ya kuulizwa
sababu za kujiuza akiwa katika hali hiyo ,
mjamzito huyo alisema hayo yote
yanatokana na ugumu wa maisha kwani
alipata mimba akiwa katika kazi hiyohiyo .
Alipoulizwa ujauzito wake una umri gani
alidai kuwa bado siku tatu tu itimie miezi
tisa akajifungue .
Aliongeza kuwa kwa sasa mmiliki wa
danguro hilo amemkataza kujiuza katika
danguro lake kwa kuwa angeweza
kujisababishia matatizo hivyo aliamua
kufanyia biashara zake nje ya danguro
hilo.
“Mbona mnanikamata jamani! Mimi sihusiki
na danguro hilo la .. .( akimtaja mmiliki)
kwanza ameshanikataza kujiuza kwenye
danguro lake kutokana na hali yangu . Yote
ni maisha tu jamani!” alisema.
Baadaye Hamisa pamoja na wenzake
walipandishwa kwenye karandinga na
kupelekwa kituo cha polisi Mbagala - Kizuiani
wakisubiri sheria ichukue mkondo wake
kwani shitaka kubwa

No comments:

Post a Comment

.