Tuesday, February 18, 2014

BABY MADAHA ATANGAZA KUACHA MUZIKI NA FILAM

IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe
katika mtego wa kujiuza na makachero wa
OFM ya Global Publishers , staa wa Bongo,
Baby Madaha ametangaza kuachana na
sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo
kuwa amechoshwa na maisha ya presha .
Baby Madaha.
Akistorisha na paparazi wetu juzikati jijini
Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile
imemsababishia matatizo makubwa ya
kifamilia na hata kibiashara , hivyo kujutia
mchezo mzima ulivyokuwa .
Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na
kibao chake cha mwisho kukitoa cha Mr. Dj
ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya
sanaa kwa upande wake .
“Nimeamua kuachana na sanaa kabisa ,
siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na
uhuru . Nitarudi kwenye fani yangu
niliyosomea ( hakutaka kutaja ) , maana
naishi maisha ambayo hayana amani
kabisa, ” alisema.
Hivi karibuni Madaha aliingia kwenye kumi
na nane za Oparesheni Fichua Maovu ‘ OFM ’
ya Global Publishers ambapo alipatana bei
ya kutoa uroda kwa ‘mfanyabiasha’ wa
madini kutoka jijini Mwanza
aliyejitambulisha kwa jina la Mike – kumbe
ulikuwa mtego .

No comments:

Post a Comment

.