Yelewiii! Dereva ‘ suka ’ wa kampuni moja
binafsi yenye makao yake makuu Kurasini
jijini Dar ( jina halikupatikana ) Jumapili
iliyopita alinaswa akifanya mapenzi na
changudoa ndani ya gari la kampuni hiyo ,
kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ( OFM)
kilishuhudia tukio hilo laivu .
Dereva ‘suka ’ baada ya kunaswa akiwa na
changu (kulia ).
Dereva huyo akiwa na mwenzake walifika
maeneo ya Mbagala Zakhem saa 7 usiku wa
Februari 16 , mwaka huu bila kujua kama
OFM ilikuwa katika maeneo hayo kwa ajili
ya kufanya oparesheni tokomeza
machangudoa.
OFM ilimshuhudia dereva huyo na mwenzake
wakishuka ndani ya gari aina ya Toyota
Hilux ( isiyokuwa na ‘ pleti’ namba upande
wa mbele ) mali ya kampuni hiyo , wakiingia
kwa fujo katika moja ya madanguro
maarufu na kupaki gari kisha wakashuka
kuelekea kwenye danguro la machangudoa.
Changu akiwa ndani ya gari .
Baada ya muda , mmoja wao alirejea akiwa
na changudoa maarufu kwa jina la
Waluwalu na kujifungia ndani ya gari hilo .
Kama kawaida yake OFM iliwataarifu askari
wa Kituo cha Kizuiani waliokuwa doria
katika eneo hilo ambao kwa pamoja
walilivamia gari na kumuamuru dereva
ashuke .
Changu pamoja na mteja wake wakiwa na
aibu baada ya kunaswa.
Hata hivyo , suka huyo alikuwa mbishi
akaamua kufunga milango na kupandisha
vioo ili asiweze kubughudhiwa na kile
alichokuwa akikifanya ndani ya gari .
Askari waliokuwa na silaha wakalizunguka
gari hilo na dereva huyo alipoona mambo
yamekuwa magumu alifungua mlango na
kutimua mbio lakini hakufika mbali kabla
ya kuwekwa chini ya ulinzi sambamba na
changudoa aliyekuwa naye .
Mwana OFM ( kushoto ) akiwa kazini baada
ya kuwanasa watu hao.
Akizungumza kwa hofu dereva huyo
alisema, yeye na mwenzake ni madereva wa
kampuni ... ( jina tunalo) na walikuwa
maeneo hayo kwa bahati mbaya na si kama
walifika kuwanunua machangu hao .
Dereva huyo alipotakiwa atoe sababu za
kujifungia ndani ya gari hilo na changudoa
kisha kutoa pleti namba ya mbele ya gari ,
alijitetea kwa kusema kuwa pleti namba
ilidondoka barabarani tangu mchana, hivyo
walikuwa wakimtafuta fundi ili
awatengenezee .
Suka na Changu wakiwa na watuhumiwa
wengine walionaswa katika operesheni
tokomeza uchangudoa .
Alipohojiwa changudoa waliyekuwa naye ,
hakuwa na lolote la kusema zaidi ya
kuangua kilio na kuomba aachiwe huku
akilaumu ukali wa maisha kama sababu ya
kujiingiza katika biashara ya kujiuza.
Wahusika hao walifikishwa Kituo cha Polisi
cha Kizuiani kabla ya kesho yake
(Jumatatu) kupelekwa Mahakama ya Jiji
kusomewa makosa yanayowakabili .
. .. Changu akishushwa kutoka kwenye gari .
Tuesday, February 18, 2014
DEREVA AFUMANIWA NA CHANGU NDANI YA GARI LA KAMPUNI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment