Tuesday, February 18, 2014

LINA SPEWA MIMBA NA MDOSI

MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya ,
Estelinah Sanga maarufu kama Linah,
anadaiwa kupewa ujauzito na kijana
mmoja wa Kihindi anayejulikana kwa jina
moja la Nagar.
Estelinah Sanga ' Linah'.
Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili
kuwa msichana huyo aliyeibukia kutoka
kituo cha kukuza vipaji cha THT, amekuwa
karibu na Mhindi huyo anayedaiwa kuishi
Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu
sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana
kumfurahisha sana msanii huyo .
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda
mrefu na inaonekana hii mimba ameipenda
sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi
wake , ” kilisema chanzo hicho kilichodai
kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana
pamoja katika sehemu mbalimbali za
starehe.
Chanzo hicho kilisema Linah alikutana na
mdosi huyo katika harakati zake za
kimuziki na kwamba jamaa ameoza mno
kwa binti huyo , mkali wa albamu ya
Atatamani.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza
hakupokea, lakini baada ya kutumiwa
ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa
kuhusu suala hilo , alipiga simu na
kukanusha vikali tuhuma hizo .
“Nani kakwambia kama nina mimba ?
Hakuna kitu kama hicho , hayo ni maneno
ya watu wanasambaza mtaani , mimi hata
sijui wananitaka nini , ” alisema.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia
habari hizo , alisema anazisikia na kusisitiza
kuwa siyo za kweli . Lakini alipotakiwa
kusema kama anamfahamu Nagar, alimtaka
mwandishi kuachana na habari hizo .
“Wewe si umeuliza habari za mimba ? Sasa
hayo mengine yanatoka wapi, ulichotaka
kujua nimekujibu , hayo mambo mengine
achana nayo , ” alisema bila kufafanua
zaidi .

1 comment:

.