MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa dansi
nchini, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’
amefunguka mazito juu ya matumizi
mabaya ya bangi na madawa ya kulevya
ikiwa ni pamoja na jinsi alivyokuwa
akiyatumia.
Ramadhan Masanja ‘ Banza Stone ’ kabla ya
kufanya mahojiano na Global TV Online.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Mtu Kati
cha Global TV Online mwanzoni mwa wiki hii ,
Banza alikiri kutumia madawa ya kulevya
na kusema ; “ Nilianza kuvuta sigara ya
kawaida, nikaja bangi na baadaye madawa
ya kulevya aina ya Heroin ambapo alikuwa
akiyatumia kwa kuchanganya na sigara au
bangi .
“Ujana ulisababisha nikajiingiza katika
matumizi ya madawa ya kulevya ila sasa
nimeacha kabisa na nawashauri vijana
wenzangu kuwa mbali na kilevi hicho kwani
kama huna kipato cha kutosha unaweza
kugeuka kibaka maana mwili ukizoea ni
vigumu kuacha . ”
Friday, February 28, 2014
BANZA : NILIANZA SIGARA , BANGI, UNGA ILA SASA …
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment