Friday, February 28, 2014

STEVE NYERERE AMWAGIA SIFA LULU


Stori : Mayasa Mariwata
RAIS wa Bongo Movie Unit, Steven Mengere
‘Steve Nyerere ’ amemmwagia sifa staa wa
filamu Bongo , Elizabeth Michael ‘ Lulu’ kuwa
ni binti mdogo lakini sasa anajitambua
tofauti na wasanii wengine wakubwa.
Elizabeth Michael ‘Lulu ’.
Akipiga stori na Ijumaa Steve alisema kuwa ,
mbali na umakini katika kazi zake za
kisanii , sasa hivi yuko makini sana na
maisha yake kiasi kwamba ni nadra sana
kumkuta na skendo za kijingajinga.
Steve Nyerere .
“Achilia mbali hao mastaa wote unaowajua
wewe, mimi nikiwa kama kiongozi wa Bongo
Movie siwezi kusema uongo , namkubali sana
Lulu kwani ni binti mdogo na anajitambua
na sasa siyo mtu wa kuendekeza mambo ya
starehe kama wengine, pia huwezi kumuona
viwanja kirahisi , katulia anafanya kazi , ”
alisema rais huyo .

No comments:

Post a Comment

.