WALE wapenzi wa muda mrefu, Luteni
Kalama na Isabela Mpanda hivi karibuni
walizinguana kinomanoma baada ya
Kalama kwenda kumchomoa kwa nguvu
mpenzi wake huyo akiwa bandari ya Dar es
Salaam alikokuwa akifanya taratibu za
kwenda Zanzibar kushuti filamu .
Luteni Kalama na Isabela Mpanda.
Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio
kilisema: “ Sisi tulishangaa kumuona Kalama
anakuja akiwa amefura, alipomuona tu
Isabela akamchukua kwa nguvu ,
walizinguana sana na baadaye wakaondoka
pamoja, hatukujua tatizo nini ila
inaonekana kuna kitu .”
Isabela Mpanda .
Baada ya kuipata ishu hiyo , mwandishi wetu
alimtafuta Isabela na alipopatikana
alisema: “ Kweli nilikuwa naenda Zanzibar
lakini mbaya ni kwamba sikumuaga ,
alipopata taarifa kuwa niko bandarini
akaja kunichomoa , lilikuwa ni tukio la aibu
sana. ”
Luteni Kalama .
Kwa upande wake Kala alifunguka kuwa,
alifikia uamuzi wa kwenda kumrudisha
baada ya kusikia anaenda kushuti filamu
Zanzibar bila kumtaarifu hivyo akaona
huko ni kuchezewa sharubu.
Friday, February 21, 2014
ISABELA MPANDA , KALAMA WAZINGUANA KINOMANOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment