Friday, February 21, 2014

SHILOLE ARINGIA ‘ UPAJA’ WAKE KWA MABUZI !


Msanii wa muziki ambaye katika siku za hivi
karibuni ameonekana kuvuma , Zuwena
Mohammed ‘Shilole ’ alijitapa kuwa na paja
la haja huku akidai ni sehemu ya mwili
inayomfanya awe na mvuto na kuwadatisha
wanaume .
Zuwena Mohammed ‘Shilole ’.
Katika tukio la hivi karibuni ndani ya Ofisi
za Global Publishers , Mwenge Bamaga jijini
Dar, alipofika kwa ajili ya mahojiano na
Global Television Online inayorushwa kupitia
mtandao wa www. globalpublishers.info ,
msanii huyo alitakiwa kupozi ili apigwe
picha lakini cha ajabu alipandisha juu
kigauni chake na kuonesha kipensi kifupi
alichokuwa amevaa huku akidai ana paja
la maana hivyo hana sababu ya kulificha .
“Mguu ninao, paja ninalo kwa nini
nijifichefiche bwana ?” Alisema Shilole na
katika mahojiano alidokeza kuwa, mabuzi
anayo na lazima ayachune kwani yeye ni
mtoto wa kike .

No comments:

Post a Comment

.