Stori : Hamida Hassan
Picha za nusu utupu ambazo amezipiga
mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate
Mwegelo zinaonekana kumtesa kufuatia
baadhi ya waumini wa kanisa analosali
kumsema kuwa anakwenda kinyume na
maadili .
Picha hizo anazoonekana amevaa gauni
refu jekundu huku likiwa na mpasuo ‘ wa
haja’ uliyolifanya sehemu kubwa ya paja
lake kuwa wazi, zimesambaa kiasi cha
kuwafanya baadhi ya mashabiki wake
kumtaka ajiangalie upya .
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati
tofauti, baadhi ya wadau wamesema
kutokana na jinsi alivyokuwa ametulia
kiimani , mrembo huyo alikuwa anaelekea
kwenye ulokole lakini kwa hili anapotea .
“Unajua yule ni modo mwenye jina kubwa
sana lakini alikuwa ametulia sana , hata
nilipomuona amejiunga na kwaya ya pale
kanisani kwetu St . Peter, niliona ameamua
kumfuata Yesu kikwelikweli lakini kwa picha
hizi, mh!” alisema Juster John anayesali
kanisani hapo .
Naye rafiki wa Jokate aliyeomba hifadhi ya
jina lake alisema : “ Ninachokumbuka Jokate
aliwahi kuniambia anataka kuokoka ili
amtumikie Yesu kisawasawa lakini kwa
mavazi haya nadhani mawazo ya ulokole
itakuwa basi tena . ”
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta
Jokate na kumuuliza juu ya picha hizo ,
alipopatikana alisema: “ Nilizipiga kwa ajili
ya kuitangaza kampuni yangu ya mitindo
ya Kidoti .
Ijumaa: Sasa mbona umeacha mapaja wazi
sana?
Jokate : Huh !
Ijumaa: Huh nini ?
Jokate : Nishasema ni za Kidoti , ilikuwa ni
kwa ajili ya kutangaza nguo na nywele
zangu .
Ijumaa: Kuokoka ndiyo basi tena ?
Jokate : Kimyaaa.
Hata hivyo gazeti hili linamshauri mrembo
huyu kwamba , kwa kuwa ameshajijengea
heshima kubwa kwenye jamii, ni vyema
akawa makini na mavazi kama haya
ambayo yanaweza kumfanya akatafsiriwa
tofauti.
Friday, February 28, 2014
JOKATE ULOKOLE BASI !
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment