Friday, February 28, 2014

WEMA AFUNGUKA

Mwanadada Wema Sepetu ambaye pia aliwahi
kuwa Miss Tanzania 2006 ambaye kwa sasa
anaendesha kampuni yake binafsi iitwayo
Endless Fame inayojishughulisha zaidi na
utengenezaji wa Filamu mbalimbali.
Kupitia kipindi cha Leo tena February 28 Wema
Sepetu amekubali kutaja sifa za mwanaume
anayempenda kuwa na mvuto kwake,swali
lililoulizwa na Watangazaji wa kipindi hicho ni
kuhusu mwanaume wa sifa gani anayedhani
anaweza kuolewa nae ambapo Wema alijibu
“Kuolewa sio shida je huyo mwanaume
nampenda,maana naweza kuja kuchumbiwa
lakini nisimpende”
“Mimi nampenda Mwanaume mweusi,wanaume
weupe sio kwamba sijawahi kuwa nao lakini
nakuwa sina mzuka nao”.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond
amekiri kwa kusema’Kweli niko na Nasib -
Diamond na nadhani muda huu kutakua na
utulivu ndani yake,ule utoto tuliokua tunafanya
nadhani ulikua utoto na imekua Power Couple
toka mwaka 2010 kwa hiyo tuna ni miaka 4
sasa,kwa sasa tumeamua kuwa serious’.
Habari kwa Hisani ya Millard Ayo
Wema Sepetu pia kaandamana na Ant Ezekiel
kwenye interview ya kipindi hicho kinachorushwa
na Clouds Fm.

No comments:

Post a Comment

.