MWANGA umeanza kuonekana juu ya kesi
inayomkabili staa wa filamu za Bongo,
Elizabeth Michael Kimemeta ‘ Lulu’ ya
kumuua bila kukusudia staa mwenzake wa
muvi , Steven Charles Meshack Kusekwa
Kanumba ambapo safari hii aliamua kukiri
vipengele kibao, Risasi Mchanganyiko lina
habari yote.
Elizabeth Michael ' Lulu' aliyeambatana na
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni ’ wakiwa eneo la
mahakama .
Akikiri mbele ya Mahakama Kuu ya
Tanzania juzi (Jumatatu) wakati kesi hiyo
ilipoanza kusikilizwa , nyota huyo aliweka
wazi mambo ambayo hapo awali hakuwahi
kuyakubali kortini jambo lililovuta hisia za
wasikilizaji waliokuwa wamefurika ndani ya
chombo hicho cha kutoa haki kujua
kinachoendelea.
Mwendesha mashitaka wa upande wa
serikali, Monica Mbogo alivitaja vipengele
kadhaa ambavyo Lulu alitakiwa kuvikana
au kuvikubali .
Lulu, mama yake mzazi Lucresia Karugila
wakiongea na mwanasheria wao , Peter
Kibatala mahakamani.
Katika kesi hiyo iliyoendeshwa kwa ustadi
mkubwa wa wanasheria kuoneshana ujuzi wa
kusoma na ‘ kubugia ’ vipengele vigumu vya
sheria, Lulu alipata wakati mgumu wa
mambo kiasi cha kumwita wakili wake , Peter
Kibatala mara kwa mara .
MADAI YA KUMUUA KANUMBA BILA
KUKUSUDIA
Lulu alikiri kwamba, mashitaka yake
mahakamani hapo yalikuwa ya kumuua bila
kukusudia, marehemu Steven Kanumba
Aprili 7 , mwaka 2012.
Lulu akiongea na mama yake kabla kesi
yake kuanza kusikilizwa.
KUWEPO ENEO LA TUKIO NA KUTOKEA KWA
UGOMVI
Katika maelezo yake, Lulu aliweka bayana
kuwa siku ya tukio alifika nyumbani kwa
marehemu maeneo ya Sinza ya Vatican
jijini Dar saa 6 usiku na kuingia moja kwa
moja chumbani .
Alizidi ‘kuchezesha taya ’ kuwa, kulitokea
ugomvi kati yake na marehemu licha ya
kutotaja chanzo cha ugomvi huo.
Aliongeza kwamba, Kanumba alimvuta
mkono na kumrudisha ndani wakati
alipokuwa akijaribu kukimbia na kuufunga
mlango , mwishowe alifanikiwa kutoka na
kukimbia kusikojulikana.
KUKAMATWA KWAKE BAMAGA
Lulu aliweka wazi kuwa, siku ya tukio , saa
11alfajiri alikamatwa maeneo ya Bamaga -
Mwenge jijini Dar es Salaam alipokuwa
akijaribu kutorokea kusikojulikana.
KUHUSU UHUSIANO
Bila kupepesa macho wala kuchezesha kope ,
Lulu alikubali kuwahi kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na marehemu Kanumba kwa
muda ambao hakuutaja hali ambayo baadhi
ya watu walionesha kuwa ‘ sapraizidi ’ .
AMWAGA MACHOZI KORTINI
Awali, Lulu alipofika mahakamani hapo
akiwa ameongozana na mama yake mzazi,
Lucresia Karugila na staa wa muvi za
Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk . Cheni ’
alionekana kuwa na amani .
Msanii huyo alimudu kusoma Gazeti la
Ijumaa Wikienda ambalo liliingia mtaani
siku hiyo . Lakini baada ya kuanza kwa kesi,
ilifika mahali alidondosha machozi hali
iliyomlazimu kujifuta uso kwa kitambaa .
Baadhi ya watu walinong’ona kuwa, mrembo
huyo alikuwa analizwa na kumbukumbu za
tukio la kifo cha Kanumba na kwa sababu
ya kuogopa kesi.
MAMA KANUMBA ASUSA
Habari nyingine zilidai kuwa, mama wa
marehemu Kanumba , Flora Mtegoa
hakutokea mahakamani hapo licha ya
umoja na udugu alionao kwa sasa na
familia ya Lulu.
Ilidaiwa kuwa sababu kubwa ya kushindwa
kufika kortini ni kukosa uamuzi wa upande
gani angekaa kati ya mshtakiwa ( Lulu) na
mshitaki ( Jamhuri) kwa vile kote kuna
muhusu kwa sasa.
“Unajua mama Kanumba alipogundua
kwamba anayetakiwa kujibu madai ni Lulu
ambaye baada ya kutoka mahabusu
alimtangaza ni mwanaye na anayelalamika
ni serikali , alishindwa kujua akija leo
(juzi ) angekaa upande gani? Akaamua
kutokufika kabisa , ” kilisema chanzo chetu.
Risasi Mchanganyiko lilimsaka kwa simu
mama huyo lakini bila mafanikio kufuatia
simu yake ya mkononi kuita muda mrefu
bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Lulu alikamatwa kwa kosa la kumuua bila
kukusudia aliyekuwa galacha wa filamu za
Kibongo, marehemu Steven Kanumba mnamo
Aprili 7 , 2012 nyumbani kwake, Sinza
Vatican jijini Dar.
Baada ya kukamatwa na kuswekwa
mahabusu ya Kituo cha Polisi Oysterbay jijini
Dar, Lulu alipandishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo hakutakiwa
kujibu ndiyo au hapana .
Hata hivyo , ilielezwa kuwa mahakama hiyo
haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ya
madai hayo.
Aliachiwa kwa dhamana Januari 29 , 2013 na
kuambiwa kwamba kesi yake itakaporudi ,
itakuwa chini ya mahakama kuu. Juzi
ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza .
Tuesday, February 18, 2014
KESI YA KIFO CHA KANUMBS LULU SONHEA UKWELI,SIKU HIYO AVAA KILOLOLE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment