Thursday, February 27, 2014

Kisa cha mtoto aliyechinjwa juzi mbagala charambe njia panda nzasa.

Kisa cha mtoto aliyechinjwa juzi mbagala charambe njia panda nzasa.Mtuhumiwa wa mauji hayo alijulikana kwa jina moja la ustadhi Ngulangwa,yasemekana aliwahi kuwa mwalimu wa madrasa aliacha kufundisha kutokana na kuwa na matatizo ya akili.Kisa hiko kilitokea juzi majira ya 5 jioni ya Tanzania,watoto wawili wa kiume wenye umri unaolingana wa miaka 9 walikua wakipita eneo la nyumba ya mgonjwa huyo,ndipo alipowaita watoto hao na bila kusita wakaenda kisha akamkamata mtoto mmoja na kumchinja na kuingia na kichwa ndani na kujifungia.Yule mtoto mwengine alikimbia huku akipiga kelele ustadhi kauwa ustadhi kauwa,ndio watu kukimbilia kuona mauji hayo na kumkuta muuaji huyo akiwa ndani kajifungia anachungulia dirishani hali ya kuwa mkononi kashika kichwa na kisu huku akisema atakaeingia ndani na yeye na mchinja.Watu wenye hasira kali walivunja mlango na kuingia ndani na kuanza kumpiga mwenye mawe,mwenye fimbo hadi kufa na yeye.

1 comment:

.