Thursday, February 27, 2014

TENA LEO BIFU JIPYA KATI YA SUPER STAR WOLPER NA YULE MWANAUME WA MICHEPUKO MANAIKI SOMA MWENYE LIVE!!


Na Sakina Shabani
Msanii nyota kwenye tasnia ya filamu za
kibongo Jacqkline Wolper na Manaiki Sanga,
anayejulikana kama The Don, wako katika bifu
kubwa kisa kikiwa ni picha walizopiga pamoja.
Tukio hilo limechukua sura mpya kwenye
mitandao ya kijamii baada ya wiki mbili
zilizopita gazeti hili kuanika picha za mastaa
kadhaa waliowahi kupiga picha zilizozua
minong’ono mitaani, kutokana na tabia ya
Manaiki kuaminika kuwa ni wanawake
aliotembea nao.
Maskani Bongo liliandika juu ya Wema Sepetu
kunasa kwenye mtandao wa ngono, huku
likionesha picha yake kubwa akiwa na Manaiki
Sanga wakiwa wamekumbatiana huku picha
ndogo ndogo za wasanii wengine maarufu
akiwemo Jackline Wolper nao zikiwaonyesha
wakiwa na mcheza filamu huyo.
Baada ya habari hiyo kutoka, baadhi ya
watumiaji wa mitandao hiyo walichukua kurasa
za gazeti hilo na kuiweka mtandaoni na watu
walipoanza kutoa maoni yao, Jack
alimzungumzia Manaiki na kukanusha kuwahi
kushiriki naye mapenzi.
Mjadala mkali ulizuka huku mashabiki wa
wasanii hao wakisemana vikali ambapo Wolper
aliomba kuelezea jinsi ilivyokuwa hadi
akakutana na Manaiki, akasema “Duh yaani
mimi nimekuwa mpenzi wa Manaiki tena? Huyu
mshikaji alishaahidi kuwa kwa gharama yoyote
atakuwa staa, hivyo akatoa mkwanja wake
watu tukaula basi,” alisema Wolper

1 comment:

.