UNAFIKI , kubaguana na upendo wa maigizo
vimeendelea kuonekana miongoni mwa
mastaa wa Bongo baada ya hivi karibuni
kususa hafla ya kumtoa nje mtoto wa
mwigizaji machachari, Rose Ndauka aitwaye
Naveen.
Tukio hilo lilishuhudiwa na kamera za Risasi
Mchanganyiko , lilitokea wikiendi iliyopita,
nyumbani kwa msanii huyo , Tandale –
Tanesco , Dar, ambapo kichanga chake
kilikuwa kimetimiza siku 40 tangu kuzaliwa
kwake.
Tofauti na matarajio ya wengi , hafla hiyo
ilihudhuriwa na mastaa wachache ambao
hata hivyo baadhi yao hawakuonesha
ushirikiano wa kutosha – ni kama
walikwenda kutembea tu!
Wengi kati ya wachache waliohudhuria
walijifungia ndani , wakikwepa macho ya
watu badala ya kusaidiana majukumu ya
hapa na pale kama ilivyotegemewa .
Wasanii walionekana kuwa bize kumuunga
mkono mwenzao ni pamoja na Yvonne
Cherry ‘ Monalisa’ , Suzan Lewis ‘Natasha ’ ,
Chuchu Hans na Skaina Ally.
Risasi Mchanganyiko lilimwuliza Rose kuhusu
kususwa huko ambapo alijibu: “Siwezi
kusema wamenisusia, unajua wakati
mwingine huenda wametingwa na
majukumu. Nilichokifanya ni kutimiza
wajibu wangu wa kuwaalika wenzangu na
nilitegemea wangenisapoti .
“Hata hivyo wapo baadhi walitoa udhuru
mbalimbali. Nimefurahi kwa waliofika na
nimefarijika sana kuja kusherehekea
pamoja nami . Nawapenda wote maana ni
ndugu zangu .”
Akaongeza: “Pia siwezi kuacha kumshukuru
mama yangu mzazi pamoja na mama mzaa
chema ( mkwewe ) kwa kunipa sapoti katika
kipindi chote nilichokuwa mjamzito mpaka
nilipojifungua salama .. . jamani mimba siyo
kitu kidogo .”
Wednesday, February 12, 2014
MASTAA WASUSA 40 YA MTOTO WA NDAUKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment