Wednesday, February 12, 2014

WASTARA ANYWA SUMU

IKIWA imetimia mwaka mmoja na miezi
kadhaa tangu kifo cha mumewe, Juma
Kilowoko ‘ Sajuki ’, staa wa filamu za
Kibongo, Wastara Juma, Jumamosi iliyopita
amedaiwa kufanya jaribio la kutaka kujiua
kwa kunywa sumu , Risasi Mchanganyiko
limefuatilia tukio hilo hatua kwa hatua.
Wastara akiwa kitandani baada ya kunywa
sumu .
KABLA YA YOTE
Awali, staa huyo ambaye amepitia mitihani
mingi , alitundika picha katika Mtandao wa
Kijamii wa Instagram na kulalamika
kuumwa tumbo .
Katika maelezo aliyoyaandika sambamba na
picha hiyo , Wastara alimshukuru msanii
mwenzake , Tamrina Poshi ‘Amanda ’ kwa
msaada aliompatia kwa kuwa alikuwa
katika hali mbaya .
SUMU YATAJWA
Siku chache baada ya kuweka picha hiyo ,
Risasi Mchanganyiko lilipata kisa kizima
kupitia kwa chanzo chake makini kuwa staa
huyo alisumbuliwa na maumivu ya tumbo
baada ya kuokolewa katika jaribio lake la
kutaka kukatisha uhai wake kwa kunywa
sumu.
SUMU ILIYOTUMIKA
Inadawa kuwa Wastara aliamua kunywa
vidonge aina ya fragile kwa kuchanganya
na pombe kwa lengo la kukatisha uhai wake
ili kuondokana na manyanyaso anayoyapa
kutoka kwa baadhi ya watu.
HAUSIGELI AOKOA JAHAZI
Inadaiwa kuwa wakati staa huyo akiwa
chumbani kwa lengo la kujiua, msaidizi wa
kazi ‘hausigeli’ aliingia chumbani humo kwa
nia ya kufanya usafi ndipo alipomkuta
Wastara akiwa analia huku amejiinamia .
“Hausigeli alijaribu kumuuliza sababu ya
kilio chake lakini Wastara hakumjibu kitu ,
aliendelea kulia bila kikomo, ” kilisema
chanzo hicho .
Inadaiwa kuwa baada ya kutojibiwa kitu ,
hausigeli huyo alitoka na kumfuata Amanda
ambaye alikuwa katika chumba kingine na
kumweleza hali aliyomkuta nayo Wastara
chumbani humo.
AMANDA APATWA NA MSHTUKO
Baada ya kuingia chumbani kwa Wastara ,
Amanda alipatwa na mshtuko mkubwa
alipomkuta shoga’ ke akiwa na baadhi ya
vidonge mkononi na kumuuliza kisa cha
kutaka kumeza vidonge hivyo .
“Wastara alimwongopea Amanda kwamba
vidonge hivyo ni kwa ajili ya kujitibia mguu
wake lakini Amanda hakukubaliana na
maelezo hayo baada ya kuiona chupa ya bia
iliyokuwa pembeni, kwa kuwa anafahamu
Wastara siyo mnywaji wa pombe, ndipo
alipobaini lengo lake la kutaka kujiua, ”
chanzo kiliendelea kushusha data hizo .
Chanzo hicho kimesema kuwa Amanda
alimpatia huduma ya kwanza shoga’ake
huyo kwa kumnunulia maziwa na kumpeleka
katika dispensari ya karibu ili kupata
matibabu zaidi ya kuondoa sumu ya vidonge
alivyovimeza.
SABABU ZA KUTAKA KUJIUA
Kwa mujibu wa chanzo kingine cha habari ,
Wastara alitaka kukatisha uhai wake
kutokana na kuchoka kunyanyapaliwa ,
kudhalilishwa na kutongozwa mara kwa
mara na wanaume , hali ambayo imekuwa
ikimfedhehesha mbele ya jamii.
Chanzo hicho kimesema kwamba kabla ya
tukio hilo , Wastara alikuwa akilalamika
kudhalilishwa na watu anaowadai fedha
zake ambao hawataki kumlipa haki yake.
“Kuna watu wengi ambao Wastara anawadai
lakini wanamsumbua kwa kumuona ni
mwanamke asiye na nguvu na wengine
wanatumia mwanya huo kumtongoza ,
mwenyewe anaamini haya yote yanatokea
kwa kuwa Sajuki hayupo, ” kimetoboa chanzo
hicho .
Habari zaidi zinadai kwamba hivi sasa
Amanda anaendelea kumwekea ulinzi wa
karibu Wastara ili asiweze kuchukua uamuzi
mbaya wa kukatisha maisha yake.
Baada ya kuyapata madai hayo, mwandishi
wetu alimpigia simu Wastara ili kupata
undani wa tukio hilo lakini kwa muda mrefu
simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
Jumapili iliyopita Risasi Mchanganyiko
lilimtafuta Amanda ili kuweza kupata
ukweli wa madai hayo na kumuuliza kama
bado yupo kwa Wastara.
HUYU HAPA AMANDA
“Wastara amepatwa na matatizo , kwa kuwa
ni rafiki yangu ambaye aliwahi kunisaidia
siku za nyuma niko naye kumfariji …”
alisema Amanda .
Risasi Mchanganyiko : Hivi amepatwa na
matatizo gani?’
Amanda: Ya kawaida tu.
Risasi: Inadaiwa kuwa amekunywa sumu ?
Amanda: Miye siyo msemaji wake , ila elewa
kuwa amepatwa na matatizo , si umpigie
kwenye simu yake uzungumze naye ?
Risasi: Simu yake haipokelewi ! Kama uko
naye karibu nipe basi nizungumze naye?
Amanda: ( kimya kidogo halafu) … Siko naye
hapa.
Risasi Mchanganyiko : Wewe uko kwa Wastara
tangu lini ?
Amanda: Nina muda kiasi kwa kuwa kuna
kazi tulikuwa tunataka kufanya.
Baada ya kuachana na Amanda , jioni ya
Jumapili iliyopita Risasi Mchanganyiko
lilimtafuta tena kupitia simu yake ya
kiganjani Wastara na kumpata.
Wastara: Haloo
Risasi Mchanganyiko : Naongea na
Wastara…?
Wastara: Eeeh ndiyo miye .
Risasi Mchanganyiko : Pole na matatizo .
Wastara: Asante , lakini nazungumza na
nani ?”
Risasi Mchanganyiko : Mwandishi wa habari
wa Global Publishers , nasikia umekunywa
sumu kwa lengo la kutaka kujiua ….
Hata hivyo , upande wa pili wa simu haukuwa
tena hewani , mlio wa kukatika kwa simu
hiyo ulisikika .
Jitihada za kumpigia simu Wastara
ziliendelea lakini hazikuweza kuzaa
matunda kwani iliita bila ya kupokelewa na
baada ya muda simu yake haikuwa
ikipatikana tena .
TUJIKUMBUSHE
Mwaka 2008, Wastara kabla ya kufunga
ndoa na Sajuki alipata ajali ya pikipiki
iliyosababisha kukatwa mguu na kuwekwa
mguu wa bandia .
Mwaka 2009, Wastara na Sajuki walifunga
ndoa ya kihistoria na kuwavutia watu wengi .
Lakini Januari 2 , 2013, staa huyo alipata
pigo la kufiwa na mumewe huyo baada ya
kumuuguza kwa muda mrefu na kuzua
simanzi kwa watu wengi .

No comments:

Post a Comment

.