Sunday, February 23, 2014

MBONGO ABAKWA CHINA , AFA


Stori : Mwandishi Wetu
AMA kweli dunia hadaa , ulimwengu shujaa !
Kumeibuka mchezo mchafu , kuna
Watanzania wanawachukua warembo nchini
na kuwapeleka China kwa ahadi kwamba
wanakwenda kufanya kazi saluni , wakifika
kule wanawanyang’ anya paspoti na kuwauza
kwa wanaume ( ukahaba ), sasa yamemkuta
Mbongo aitwaye Sabrina au Habiba , Ijumaa
Wikienda lina mkasa wa kusikitisha .
Habari za uhakika kutoka kwa chanzo chetu
nchini humo zilisema kuwa, Sabrina (24 ) ,
alifariki dunia Alhamisi iliyopita kufuatia
kubakwa na wanaume watano , raia wa
Nigeria ambao wamo nchini humo kibiashara.
Tukio hilo lilijiri kwenye hoteli moja iliyopo
kwenye Mji wa Guangzhou ambao umejaa
wageni wengi , wakiwemo Watanzania .
SIKU YA TUKIO
Rafiki wa karibu wa Sabrina, Saada alisema
siku ya tukio, marehemu akiwa katika
harakati zake za kutafuta wateja
alikutana na Mnigeria mmoja ambaye
walipatana kulala wote kwa usiku mzima .
“Kumbe yule Mnaigeria alikuwa na wenzake
wanne . Usiku walimwingilia wote kwa nguvu
kwa kumbaka mpaka akapoteza maisha
palepale. Ni ukatili mkubwa.
“Wale watu walipogundua Sabrina amekufa
waliuchukua mwili wake na kuutupa chini
kutoka ghorofa ya tano , ” alisema rafiki
huyo .
MAITI YAKUTWA HAINA FIGO , MOYO
Habari zaidi zilidai kuwa mpaka juzi
(Jumamosi ) madaktari waliokuwa
wakiuchunguza mwili wa Sabrina waligundua
hauna figo na moyo, jambo linalozidi kuzua
hofu juu ya muaji yake.
NI BIASHARA ILIYOIBUKA CHINA?
Ilidaiwa kuwa nchini China imeibuka
biashara ya viungo mbalimbali vya
binadamu ambapo ili vipatikane ni lazima
mwenye viungo hivyo auawe kwa njia yoyote .
SABRINA AFA , MGANDA APOTEA
Mtoa habari wetu alisema wakati Wabongo
wakiwa kwenye maombolezo ya kifo cha
Mtanzania huyo , mrembo mwingine raia wa
Uganda , nchi ambayo imo ndani ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki amepotea katika
mazingira ya kutatanisha nchini humo.
Baadhi ya watu wana wasiwasi kuwa kupotea
kwa msichana huyo kunahusiana na
kushamiri kwa biashara ya viungo vya
binadamu.
SABRINA ALIKWENDAJE CHINA ?
Mwezi Julai , mwaka jana , Sabrina
alikwenda nchini humo akidanganywa na
mwanamke mmoja kwamba atapata kazi
kwenye saluni ya wanawake lakini baada ya
kufika alijikuta akiingizwa kwenye biashara
ya ukahaba bila ridhaa yake mpaka
alipokutwa na mkasa huo uliopoteza maisha
yake.
TAHADHARI KWA WAREMBO WANAOKWENDA
CHINA KUFANYA KAZI SALUNI
Imebainika kuwa, kumeibuka wimbi la
Wabongo wanaofanya ‘uwakala ’ wa
kuwachukua wasichana wa Kitanzania kwa
kuwadanganya kwamba wanakwenda
kufanya kazi za saluni nchini humo.
Mara baada ya kufika , wasichana hao
hunyang’anywa paspoti ili washindwe
kuondoka nchini humo na kushinikizwa
kujiuza ( ukahaba ) huku waliowapeleka
wakipokea fedha kutoka kwa wateja .
KUIKOMBOA PASPOTI
Habari zilisema kuwa mhusika hurejeshewa
paspoti yake baada ya malipo yake kwa
‘wakala ’ kufikia dola za Marekani 8 , 000
(kama shilingi milioni 12) , ndipo huachiwa
‘huru ’ kuendelea na maisha yake.
Wengi wakishaachiwa hushindwa kurejea
Bongo na kujikuta wakiendelea kuuza miili
katika mahoteli na klabu huku wakikutana
na majanga mbalimbali.
MASOGANGE, KAJALA NA DIDA
Watanzania waishio nchini humo
wamewatahadharisha mastaa wa Bongo,
wakiwemo Mtangazaji wa Radio TimesFM ,
Khadija Shaibu ‘Dida ’ , msanii wa filamu
Kajala Masanja na Video Queen Agnes
Gerald ‘Masogange ’ ambao hupenda kwenda
nchini humo kwa shughuli zao, kutokubali
kuwa karibu na mawakala wa kuchukua
wasichana Bongo kwa kuwadanganyia kazi
ya saluni kwani wanaweza kujikuta pabaya
siku moja .
DIDA
Ijumaa Wikienda lilimsaka Dida siku ya
Jumamosi iliyopita na kumuuliza kuhusu
kuwepo kwa mawakala hao ambapo alikiri
kusikia huku akisema warembo wenyewe
wanapaswa kuwa macho na udanganyifu
huo.
“Najua wapo Wabongo wanaofanya shughuli
hiyo , si China tu hata India , unapelekwa
kwa ahadi ya kazi ya saluni , ukifika hamna
cha saluni wala nini ? Warembo wawe makini
jamani, nenda China kama una uwezo wako
mwenyewe kufanya ‘shoping ’ lakini si
kupelekwa, ” alisema Dida .
BALOZI WA TANZANIA - CHINA
Juzi , Ijumaa Wikienda lilimtafuta Balozi
wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali
Mstaafu Abdulrahman Shimbo ili azungumze
lolote kuhusu tukio la Sabrina, lakini simu
yake ilionekana kutokuwa hewani kwa muda
mrefu.
GLOBAL BADO KAZINI
Magazeti Pendwa ya Global Publishers
yanaendelea kuifuatilia habari ya kifo cha
Sabrina na yatakuwa yakiwapa wasomaji
wake kadiri kitu kipya kinapopatikana .

No comments:

Post a Comment

.