Stori : Richard Bukos
MAHABA ? Prezidaa wa Bongo Movie Unity,
Steven Mengere ‘ Steve Nyerere ’ na mwigizaji
mwenzake , Salama Salmin ‘Sandra’
wamezua minong ’ ono kufuatia kitendo chao
cha kugandana kama ruba ukumbini.
Tukio hilo lilichukua nafasi kwenye uzinduzi
wa filamu tatu za Kiswahili ‘ Swahiliwood’
kwenye Ukumbi wa Century Cinemax ,
Oysterbay jijini Dar wikiendi iliyopita.
Katika tukio hilo , wakiwa ukumbini hapo
wawili hao karibu muda wote walionekana
wakipozi kimalavidavi huku Steve Nyerere
akikumbatia ‘ pimajoto ’ la mwanadada
huyo , ishu iliyosababisha wapiga chabo
kuanza kuwajadili .
Hawakuishia hapo kwani wakati wa
vitafunwa, wawili hao walionekana
‘wakishea ’ kwenye sahani moja huku shosti
mmoja wa Sandra akiwafuata kwa nyuma
na kuwamwagia sifa kwa namna
walivyopendeza .
Kufuatia tukio hilo , ‘kachero’ wa Oparesheni
Fichua Maovu (OFM ) alianza kuwafuatilia
na kuwafotoa picha kadhaa lakini wawili
hao walionekana kutojali na wakati
mwingine waliweka pozi tata.
Juhudi za OFM kupata undani juu ya
ukaribu wa mastaa hao ziligonga mwamba
baada ya kutaka waachwe wapumzike.
Katika hafla hiyo , filamu zilizozinduliwa ni
Network , Mdundiko na Sunshine chini ya
Kampuni ya Pron Promotions Production
huku shughuli hiyo ikuhudhuriwa na mastaa
kibao wa Kibongo.
Sunday, February 23, 2014
STEVE NYERERE , SANDRA WAGANDANA KAMA RUBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment