Stori : Waandishi Wetu
ILE skendo ya kukithiri kwa baadhi ya
mastaa Bongo kujiuza imechukua sura mpya
kufuatia msanii wa Bongo Movies , Isabella
Francis ‘ Vai wa Ukweli’ naye kunasa
mtegoni, Ijumaa lina kisa kizima .
Vai wa Ukweli akiwa mawindoni.
Tukio hilo la aibu kwa tasnia ya sinema
nchini lilijiri usiku wa kuamkia Jumanne
iliyopita, Sinza ya Vatican jijini Dar es
Salaam ambapo baada ya kuumbuka , Vai
alijikuta akiangua kilio na kuomba siri hiyo
isisambae.
VAI WA UKWELI NI NANI ?
Vai ni msanii wa filamu za Kibongo kwa
muda mrefu. Amecheza filamu kadhaa
zikiwemo Beautiful Liar ( ya kwake
mwenyewe) , Family Apart , Good Fellow na
nyinginezo .
Vai wa Ukweli akificha uso wake baada ya
kunaswa .
MALALAMIKO KWA OFM
Ikiwa katika kutega ‘ rada’ zake, Oparesheni
Fichua Maovu (OFM ) ya Global Publishers
ilipokea malalamiko ya listi ya wasanii wa
kike wa Bongo Muvi wakidaiwa
kujishughulisha na uuzaji wa miili huku jina
la Vai likiwa miongoni mwao .
MCHEZO WAANZA
Kilichofanyika , Vai aliwekewa mtego na
kujikuta akiingia mzimamzima. Fuatilia
uhondo wa mawasiliano kwa njia ya ujumbe
mfupi wa maneno ( SMS, tunazo ):
OFM: Mambo Vai ? Naitwa Salum, natokea
Arusha ila kwa sasa nipo Dar, naomba
kuonana na wewe .
Vai : Ili ?
OFM: Kusema kweli nimetokea kukupenda,
nimetafuta namba yako nikaipata nikaona
nikutafute.
Vai : Muda sina.
OFM: Please usiniangushe , nitakupa chochote
utakacho, nakuomba.
Vai : Nani kakupa namba yangu ?
OFM: Sijakuelewa .
Vai : Umetumwa wewe , siyo bure.
OFM: Hivi mtu unaweza kutumwa kumpenda
mtu jamani? Usinifanyie hivyo , nipe hiyo
nafasi Vai , utafurahia.
ANAINGIA, ANATOKA
Vai : Oke , kwa nafasi umechelewa maana boy
ninaye. Kwani umefikia wapi ?
OFM: (OFM yamdanganya) niko hoteli moja
inaitwa Lunch Time hapa Tip Top Manzese
(Dar) , wewe uko wapi?
Vai : Mwananyamala (Dar) , njoo nikuone.
OFM: Nimekuja huku Kariakoo kufungasha
mzigo, we huwezi kuja pale hotelini
baadaye ? We si ni mwenyeji sana Dar?
Vai : Siwezi .
OFM: Sa tunafanyaje wangu ? Nitaumia sana
kama nitaondoka bila kukuona , nakupenda.
Vai : Ndo hivyo ukiweza njoo Mwananyamala .
OFM: Huko mimi ni mgeni wangu , nitalipia
gharama zako, usininyong’ onyeshe .
Vai : Tuma hela ya Bajaj kwa …( unatajwa
mtandao) nitakuja.
OFM: Sawa nitakutumia, ni shilingi ngapi
kutoka huko hadi hapa hotelini ?
Vai : Kumi na tano tuma .
OFM: Sawa na ofa yako tukionana ni shilingi
ngapi?
Vai : Ofa ya nini?
OFM: Si tukionana jamani ili nijiandae
nisije nikaumbuka, unajua tena watu kama
nyie…
Vai : We sikuelewi kwani kuna nini tofauti,
kuonana umetaka nimekubali bado
unaongea tofauti.
OFM: Tofauti vipi jamani?
Vai : Unazingua .
OFM: Nazingua vipi?
Vai : Tuma hiyo hela nije .
OFM: Pesa ya kujia siyo ishu , natuma twenty
(20 , 000) , nataka kujua shilingi ngapi
utataka kuwa na mimi kwa leo ili nijiandae
wangu, naomba uelewe.
Vai : Tutaongea usijali .
OFM: Kwa hiyo wangu, niambie basi .
Vai : Usijali nikija tutaongea .
OFM: Nataka ukija nisisumbuke , we niambie
tu unataka shilingi ngapi kwa kuwa na wewe
leo , nataka nikachukue pesa ATM , we mtu
mzima bwana !
Vai : Oke siwezi , achana na mie. By the way
mimi sijiuzi.
OFM: Siyo suala la kujiuza Vai , kama
unataka nikukose sawa lakini ningefurahi
sana, kuwa nawe, acha pesa, nitakupa
utakachotaka .
Vai : Siwezi .
OFM: Usinifanyie hivyo utaniumiza.
Vai : Si nimekuambia tuma nauli nije ?
Tutaongea hujiamini .
OFM: Ujue nakuuliza hivyo ili nijipange hata
kama ni kuchukua pesa nichukue za kutosha
kwa leo .
Vai : Kama huelewi basi .
OFM: Kama sielewi nini? We niambe tu.
Vai : Milioni .
OFM: Milioni moja ?
Vai : Ndiyo .
OFM: Usikomae Vai , nimetumia pesa nyingi
kufungashia mzigo , nifanyie fea wangu.
Hiyo m moja tutalala?
Vai : Siwezi .
OFM: Huwezi kulala ? Sikia , nifanyie laki
tano basi , ila itakuwa poa kama tutalala
maana mshikaji niliyekuja naye kaondoka
leo .
Vai : Kulala siwezi .
OFM: Kwa mfano kuanzia saa moja mpaka
saa ngapi hivi naweza kuwa na wewe ? Labda
nikuambie ukweli, kwa nini nimekutafuta ,
kuna picha yako niliichukua kwenye gazeti
nikakupenda sana, nikawa namaliza shida
zangu , nimekuja Dar ndo nikasema
nikutafute unipe live kwa gharama yoyote
Vai .
Vai : Kimya.
OFM: Subiri kidogo wangu nakutumia.
Vai : Mh ! Kwa nini muda unaenda , kama
umebanwa basi siku nyingine .
OFM: Noo please kuna mtu nimemwambia
akutumie 15 (15 , 000/ =) sasa hivi wangu ,
mambo mengine ukija , ukiipata niambie,
sawa ee ..
Vai : Mh !
OFM: Nini jamani tena ?
BAADA YA DAKIKA NANE
Vai : Oke nimekuelewa . Nimeipata
OFM: So unatoka huko saa ngapi? Kwani ni
mbali ?
Vai : Ndiyo , wewe uko wapi?
Vai : Nikija sitaki uswahili, mie naogopa
magazeti, sawa kaka, sasa unanipa changu
nafanya kazi yako .
Vai : Nipigie .
Vai : Uko kwa wapi maana mimi nipo Vatican
(Sinza , Dar) .
KABANG !
Baada ya kuchati kwa muda mrefu bila
kujua anaingia mtegoni, hatimaye Vai
alifika kwenye Kituo cha Daladala Vatican
lakini hakutaka kushuka kwenye Bajaj .
Badala yake alimtaka kachero wetu ambaye
ni Salum wa bandia kuingia kwenye usafiri
huo kisha akamuongoza dereva kuelekea
Baa ya Mawela iliyopo jirani na eneo hilo.
Akiwa amejiaminisha kuwa analamba laki
tano yake, Vai alianza kuagiza pombe za
bei mbaya huku akisisitiza kupewa chake
kwanza ili akampe huduma .
HALI YABADILIKA GHAFLA
Hata hivyo , hali ilibadilika ghafla , hebu
fuatilia mazungumzo yao:
Vai : Vipi mbona kama hujiamini? Kabidhi
laki tano yangu kieleweke .
Kachero wa OFM : Vai sikiliza , mimi si
pedeshee wala mfanyabiashara wa Arusha.
Ni kachero wa OFM (Oparesheni Fichua
Maovu) ya Global Publishers . Tunafichua
uovu ndani ya jamii.
Vai : ( huku akihamaki ) kaka hebu nioneshe
‘toileti’ zipo wapi hapa?
Kachero wa OFM : Toileti zile pale .
Vai alikwenda toileti ambako alikaa huko
takriban dakika tatu . Cha ajabu, alirejea
akiwa analia ambapo mambo yalikuwa hivi:
Vai : Unasema wewe ni mwandishi wa Global?
Si kweli , nawajua wote ila wewe siyo !
Kachero wa OFM : Unatakiwa kusadiki haya
niyasemayo .
Vai : Kama kweli nioneshe kitambulisho.
Kachero wa OFM : ( huku akikitoa ) hiki hapa .
Vai : Hamna . Kama ni kweli niitie Sifael
(Paul) na Erick ( Evarist ) waje hapa.
Kachero wa OFM : Hakuna shida Vai , twende
ofisini Bamaga - Mwenge wamejaa tele usiku
huu.
Baada ya kusikia hivyo , Vai alinyanyuka na
kwenda eneo la kuegesha magari na kuzua
tafrani , ndipo kijana mwingine wa OFM
aliyekuwa akilinda usalama wa mwenzake
akatoa vifaa vyake vya kunasia matukio
ambapo alimrekodi Vai akizua timbwili bila
kujua.
Mbele kidogo ya baa hiyo , Vai aliita Bajaj
na kumwagiza dereva amkimbize Global
Publishers .
Alifika kwenye ofisi za gazeti hili akiwa
anahema mithili ya mbogo aliyejeruhiwa
ambapo alitulizwa na wahariri waliokuwa
mzigoni na kufanya mahojiano :
USO KWA USO NA WAHARIRI
Wahariri: ( wakijifanya hawaelewi chochote)
nini kimetokea Vai ?
Vai : Ninyi mnajua kila kitu . Kwa nini
mmeniwekea mtego ? Kuna jamaa anadai ni
mwandishi wenu , alijifanya
mfanyabiashara akawa anawasiliana na
mimi.
Wahariri: Mlikuwa mnawasiliana kuhusu
nini?
Vai : Alisema sijui aliniona kwenye gazeti
akanipenda , amekuja Dar akaamua
kunitafuta .
Wahariri: Kukutafuta kwa nini ?
Vai : Alitaka akalale na mimi kwa laki tano .
Vai : Tulikubaliana tukutane lakini mimi
sikuwa na mpango wa kwenda kulala naye .
Nilitaka nichukue hiyo laki tano yake nimpe
sababu za ‘kiwanawake ’ so nisingefanya
naye ngono.
Wahariri: Ina maana huwa unafanya hivyo ?
Huoni hatari kuchukua fedha ya mtu na
kuingia mitini? Huo si ni utapeli? Huogopi
kutafutwa na kufanyiwa kitu mbaya ?
Vai : Naamini angenielewa tu ( kilio
mfululizo) .
STEVE NYERERE , MTITU
Baada ya Vai kukiri kuingia kwenye mtego
wa kujiuza, gazeti hili liliwasiliana na
baadhi ya viongozi wao kuwasikia
wanalizungumziaje tukio hilo .
Steven Mengere ‘ Steve Nyerere ’, Mwenyekiti
wa Bongo Movie Unity alisema:
“Tunawafukuza wote mnaowanasa , hawana
sifa ya usanii , wanaingia kutimiza ndoto
zao za kujiuza. Hawafai Bongo Muvi. ”
Naye Katibu wa Bongo Movie Unity, Wiliam
Mtitu alifunguka : “Tutakaa kikao
tumfukuze Bongo Muvi , ametuchafua sana. ”
Mmoja wa mastaa ambaye hakutaka
kutajwa jina alidai kuwa umefika wakati
kwa mastaa kujilinda wakitajwa warembo
kama Wema Sepetu, Jokate Mwegelo ,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ , Aunt Ezekiel,
Jacqueline Wolper na wengine kwamba siku
wakinaswa itakuwa ni aibu kubwa.
WENGINE KWENYE ‘TAGETI’
Listi ya mastaa wanaojiuza kwa mapedeshee
iliyopo mikononi mwa OFM ni ndefu, kikosi
bado kiko mzigoni kuwanasa .
KAZI NZURI YA OFM
Tangu OFM imeanza kazi yake nzuri ya
kufichua maovu , kabla ya Vai tayari
ilishawanasa mastaa watatu wa Bongo Muvi ,
Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz ’ , Lulu
Semagongo ‘ Aunty Lulu ’ na Baby Joseph
Madaha.
Friday, February 21, 2014
MSANII BONGO MUVI ANASA KWENYE MTEGO WA KUJIUZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment