Friday, February 28, 2014

RED HANDED ! NJEMBA AUVAA MTEGO AKIWA NA MKE WA RAFIKI YAKE GESTI


MAANDIKO yanasema ‘ usitamani mali ya mtu
mwigine’! Ni kweli kabisa, onyo hilo
lilichukua fursa yake kufuatia njemba
mmoja aliyejulikana kwa jina la Anton
John Mwaweje kunaswa laivu gesti na mke
wa rafiki yake aliyefahamika kwa jina
moja la Chalz.
Mke wa mtu sumu: Anton John Mwaweje
baada ya kunaswa akiwa na mke wa rafiki
yake gesti .
Tukio hilo lilijiri mwanzoni mwa wiki hii
kwenye gesti moja maarufu (jina tunalo)
iliyopo Buguruni - Malapa jijini Dar es
Salaam.
Katika sakata hilo ilidaiwa kuwa, Mwaweje
alikuwa akiifahamu vyema familia ya Chalz
sambamba na mke wake ( jina lipo ) lakini
hilo hakulijali na kumtokia mke wa Chalz
ambaye kwa utamaduni wa Kiafrika ni
shemejiye .
Mshangao : Anton John akishangaa baada
ya kuba
Habari zikazidi kudai kwamba, ilifika
mahali katika kumtaka shemejiye huyo
ambaye alikuwa akimkatalia katakata,
Mwaweje alitumia gia nyingine ikiwemo ya
kumuahidi mambo manono kama angekubali
kuivunja amri ya 6 ya Muumba na yeye.
Chanzo cha habari kiliendelea kudai kuwa,
‘Mungu si Athuman wa Lucas ’ siku isiyo na
jina jamaa alimtumia ujumbe ( SMS) mke
wa mwenzake kwa kutumia maneno ya
kumtoa nyoka pangoni kumbe muda huo
bwana simu alikuwa nayo mwenye mke .
Chalz alimwita mkewe na kumuuliza ni nani
aliyemtumia ujumbe huo? Ndipo mke
akaanika ukweli akisema :
“Mume wangu , wala usikonde . Aliyetuma
ujumbe huo si mwingine , ni Anton …”
Mume: “( akihamaki ) Anton huyuhuyu ?”
Mke: “Huyuhuyu mume wangu. Amekuwa
akinitaka kimapenzi kwa muda mrefu sana ,
namkatalia lakini hasikii .”
Pia , mwanamke huyo alimwonesha mumewe
meseji kibao ambazo jamaa huyo amekuwa
akimtumia na zile ambazo yeye amekuwa
akimkatalia.
“Sasa sikia, mkubalie , ” mwanaume huyo
alimwambia mke wake huku midomo
ikimcheza kwa hasira .
Chini ya usimamizi wa mumewe, mwanamke
huyo aliwasiliana na Anton na kumwambia
alikuwa na nafasi wanaweza kukutana kwa
ajili ya kumsaliti Chalz .
Baada ya kupanga mipango ya kukutana,
mume huyo alipiga simu Global Publishers
kwenye kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu
(OFM ) na kuomba msaada wa fumanizi
ambapo alibahatika kukuta kuna kamera
mpya zimewasi tayari kwa kazi kama hizo .
Baada ya kupata maelezo ya Chalz, OFM
ilishirikiana na Jeshi la Polisi Buguruni –
Kwamnyamani jijini Dar na kuandaa mtego
ambapo Jumatatu iliyopita , saa nane na
ushee mchana, Anton ambaye naye
inasemekana ana mke aliuingia mtego na
kunasa kwenye chumba namba 5 akiwa na
mke mwema huyo .
Ndani ya chumba hicho , Anton alikutwa na
boksa tayari kwa mlo wa wizi ambao
alibakia kuendelea kusikia njaa . Mezani,
kulikuwa na chipsi kuku na pombe ambazo
zingewapa stimu kabla ya mchezo .
Kitendo cha Chalz kumnasa jamaa huyo na
mkewe kitandani kilimpandisha munkari
ambapo nusura afanye ndivyo sivyo lakini
alitulizwa na polisi waliokuwa eneo hilo kwa
ajili kulinda usalama .
Kilichofuata baada ya hapo , mgoni huyo
akiwa na pingu mkononi alipelekwa kwenye
kituo hicho cha polisi ambapo awali, Chalz
alitoa ripoti ya malalamiko baada ya
kugundua jamaa huyo anataka
kumtumbukiza mkewe kwenye mstari wa
usaliti.
Mpaka OFM wanaondoka kituoni hapo ,
taratibu za kisheria kuhusiana na kesi hiyo
zilikuwa zikiendelea huku mgoni huyo akiwa
chini ya ulinzi mkali.

No comments:

Post a Comment

.