Friday, February 28, 2014

UKIKUTANA NA MTU HUYU, KAA MBALI !


Kuna mtu mmoja almaarufu kwa jina la
Kamanda au Kachero wa OFM (Oparesheni
Fichua Maovu) ya Global Publishers ambaye
unashauriwa ukikutana naye kaa mbali ,
pata undani wake .
Kamanda au Kachero wa OFM ( Oparesheni
Fichua Maovu ) .
Jamaa huyo hatari amedhamiria kuibadili
Tanzania kimaadili kwa kuibua na kufichua
uovu katika jamii.
Tayari amefanya matukio mengi makubwa
ya kufichua uovu ndani na nje ya Jiji la
Dar.
KIVIPI?
Anachokifanya Kamanda wa OFM ni kwamba
hupokea ujumbe wenye harufu ya uovu au
kero katika eneo la mtumaji kwenye
magazeti ya Global Publishers kisha
huifanyia kazi .
Baada ya kupokea ujumbe wa aina hiyo
kwenye namba zilizopo kwenye magazeti
hufanya uchunguzi wa kina usiku na
mchana.
Kamanda wa OFM akishajiridhisha kuwa
uovu huo unatendeka hujipanga kwa
kuandaa mwongozo (script ) ili kufanya
oparesheni na kuuanika uovu huo.
USHUHUDA WA BABA JOY
“Ukweli ni kwamba jamaa huwa hakurupuki
na huwa hakosei . Usiombe ukutane naye au
akufuatilie . Jamaa ni mtu hatari lakini
alinisaidia sana .
“Ndoa yangu ilikuwa ivunjike lakini
alimfuatilia mke wangu hadi nikapata
ushahidi kwani mama watoto alikuwa
akikataa katakata kuwa hanisaliti .
“Kweli baada ya kupata ushahidi mke wangu
alikiri na kuomba msamaha na sasa maisha
yanaendelea . Mimi namvulia kofia
Kamanda wa OFM , ” alisema Baba Joy ,
mkazi wa Sinza , Dar.
Mke wa Baba Joy (Mama Joy) aliwahi
kunaswa na Kamanda wa OFM kwenye
jaribio la kusaliti ndoa na mwanaume
mwingine kwenye gari .
MATUKIO YA KUKUMBUKWA YA KAMANDA WA
OFM
Yapo matukio mengi yaliyotekelezwa na
Kamanda wa OFM na hapa tunakukumbusha
machache ;
DOKTA MAMBO
Mapema mwaka huu Kamanda wa OFM
alifanikisha tukio la kunaswa kwa daktari
aliyejulikana kwa jina moja la Mambo
maarufu sana kwa jina la Dokta Mambo
ambaye alikutwa katika jaribio lililodaiwa
kuwa ni la utoaji mimba .
Wakati Kamanda wa OFM akichora ramani
ya namna ya kumnasa dokta huyo kwenye
zahanati yake iliyopo Kawe jijini Dar, watu
wengi hasa wanawake walidai jamaa huyo
hanasiki lakini alinaswa hivyo kutibu
‘ugonjwa ’ wa utoaji mimba .
BABU NA DENTI
Wiki kadhaa zilizopita , Kamanda wa OFM
alimnasa babu aliyetajwa kwa jina moja la
mzee Omari , akiwa gesti na denti wa shule
moja ya sekondari jijini Dar ( jina la denti
na shule vinahifadhiwa kimaadili) .
Tukio hilo la aibu lilijiri kwenye gesti moja
iliyopo maeneo ya Kawe, Dar na kusababisha
timbwili zito hivyo kuibua na kukemea ile
tabia ya ‘vibabu ’ kupenda kutembea na
dogodogo.
MFANYABIASHARA WA MAGARI
Tukio lingine la kuibua maovu , hivi karibuni
Kamada wa OFM alifanikiwa kumnasa
mfanyabiashara maarufu wa magari jijini
Dar, aliyefahamika kwa jina moja la
Juvenali akiwa katika jaribio la ulawiti kwa
‘modo ’ maarufu Bongo ( jina tunalihifadhi ) .
KAUMBA , MOROGORO
Kwa kushirikiana na polisi , hivi karibuni
Kamanda wa OFM alitinga mkoani Morogoro
ambapo alifanikisha kufumuliwa kwa eneo
korofi kwa biashara haramu ya ngono la
Kaumba na kwenye malori pale Msamvu .
MKE WA RAFIKI
Ukiangalia ukurasa wa nyuma wa gazeti
hili , Kamanda wa OFM amefanikisha
kunaswa kwa mwanamke mmoja aliyekuwa
kwenye jaribio la kusaliti kwa rafiki wa
mumewe ambaye pia ni rafiki wa mume wa
aliyenaswa.
KAZI NDIYO IMEANZA
Akizungumzia kazi yake hiyo ya kufichua
maovu , Kamanda wa OFM alikuwa na haya
ya kusema : “Ndiyo kwanza kazi imeanza.
“Kwa yeyote mwenye taarifa ya uovu au
ufisadi unaofanyika awasiliane na mabosi
zangu kupitia namba zao kwenye magazeti .
“Nikishainyaka hiyo taarifa , nawaahidi
kuwa sikosei , nitawafanyia Watanzania kazi
nzuri. Nimepania kuibadili Tanzania kwa
kuwa uovu unazidi kuongezeka kila
kukicha .”

No comments:

Post a Comment

.