Thursday, February 27, 2014

SIKU MASHOGA WOTE WA TAIFA WALIPOTAJWA KWA MAJINA YAO KWENYE ORODHA MAALUM ONA HAPA LIVE!!


Siku chache tu baada ya Rais wa Uganda,
Yoweri Kaguta Museven kusaini ili kuidhinisha
sharia mpya ya kupinga ushoga na shughuli
zinazohusiana na ushoga, gazeti moja nchini
humo limechapisha orodha ya “mashoga 200”
raia wa nchi hiyo siku ya jumanne wiki hii.
Gazeti la Red Pepper, linalofanya shughuli
zake katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala,
limechapisha orodha ndefu ya majina, huku
wengine wakiwa na picha zao chini ya kichwa
cha habari “EXPOSED” (waanikwa).
Katika taarifa hiyo pia kuna jina la mchungaji
wa kanisa katoliki, msanii wa muziki wa hiphop,
na mwanaharakati maarufu wa ushoga nchini
humo, Pepe Julian Onzieme. Inadaiwa baadhi
ya waliotajwa humo hawakuwahi kujitangaza
kuwa ni mashoga.
Taarifa hiyo imekuja muda mfupi tu baada ya
serikali ya Uganda kutangaza sharia mpya
ambayo inafanya shughuli zote za ushoga kuwa
ni kosa.
Pamoja mataifa mbalimbali duniani kupiga
vita hatua hiyo iliyopitishwa Uganda na vitisho
mbalimbali vya nchi ya Marekani kwa Uganda
vya kukata misaada, Rais Yoweri Museveni
alisisitiza kuwa ni muhimu pamoja na
kuingiliwa mambo yake na nchi za magharibi.
Museveni alikaririwa jumatatu akisema “Nini..!,
wanafanya(mashoga) mambo ya ajabu” na
kueleza kuwa wanatia “kinyaa.”

No comments:

Post a Comment

.