Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini
sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa
wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi
au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha
zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi
fupi sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana
au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao
hadharani na kusababisha hisia za kingono .
Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo
zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya
mafunzo au wakati wa michezo na hafla za
kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini
Kapmala, waziri wa maadili na utawala bora,
Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais
Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi
huu, miezi mwili bada ya bunge kuipitisha.
Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya
vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza
sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwa picha, au
video zenye watu uchi zinanaswa na kuharibiwa.
Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika
sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na
utumbuizaji.
Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote
atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya
watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona
sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha picha
za watu walio uchi kwa lengo la kuleta hisia
tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu
kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia
zisizofaa miongoni mwa watu.
Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia
visivyo watafungwa hadi miak 10 na wale
watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto
katika biashara ya ngono watafungwa hadi
miaka 15.
Wednesday, February 19, 2014
UGANDA YATANGAZA MARUFUKU KUVAA MINI,RAIA WAANDAMANA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment